Ni swali tu,
Salaamu wanaJF,
pili salamu ziwaendee wanausalama wa Taifa letu, awali niwapongeze na kuwapa pole kwa kazi nyingi na nzuri, lkn niseme tu nzuri zile tu mlizofanya kwa uaminifu kulinda usalama wa taifa letu, bila kutanguliza maslahi binafsi kwa gharama ya uhai wa Tanzanzia.
Sote tunakumbuka hivi karibuni tulikutwa na matukio mbalimbali ya kugusa kustua usalama wa watanzania.
Lakini bila kurefusha linalonigusa zaidi ni tukio lile la watu wasiofahamika kuwaua na kuwanyang'anya silaha polisi katika matukio mbali mbali, ambayo nadhani hadi leo hayana jibu.
Tumesikia matamko mbalimbali kuwa waliohusika na uhalifu huo wangekamatwa mara. Lakini hadi leo ni zaidi ya miezi, tangu tukio la kwanza hakuna hata silaha moja iliyokamatwa, hakuna hata mtu mmoja wa wahusika aliyesemekana kukamatwa, hatujui wahusika.
Hatujui serikali pamoja na wanausalama, au kupitia kwa wanausalama wanafanya mikakati gani kutuhakikishia usalama wetu. Hatujui wahusika wa uhalifu watafanya tukio lingine lini la mauaji wa polisi na kunyang'anya silaha tena. Mungu aliepushe hiyo mbali.
Lakini najiuliza tu, tupo salama kweli? Wanausalama wa Taifa mmeridhika na hali hiyo?
Siamini kama uwezo na ujuzi wenu unazidiwa na vibaka. Siamini kama mnashindwa kutumia mbinu zenu zote za ujuzi na uzoefu kuwakamata wauaji wa polisi, na zaidi waliopora silaha, kwani watatumia kwa uhalifu unaofuata wa raia wengine. Sipendi kuendelea lakini niseme wazi kuwa inaniuma.
Sitaki nigusie haya matukie mengine kuwa wamekamatwa sijui morogoro, mara matukio ya Amboni, maana haya hata bado ni kitendaliwili, na kama ni ya kweli? Usalama wa watanzania upo wapi ikiwa Alshabaaba wanafika hadi kilombero na silaha kali za kivita?
Inaniuma zaidi pale ambapo maslahi binafsi yanaingizwa kwa gharama ya maisha ya m/watanzania.