Hii kitu imekaa njema sana. kidogo kidogo tutafika. Sasa kama watu wanamiliki simu za mikononi hadi vijijini, mitandao ipo sio kama zamani hadi upande juu ya mti, babu yangu kule kijijini ana kisimu chake na maisha yanakwenda, wewe Radhi unataka mtanzania wa kawaida imfikie vipi? Labda utoe mawazo yako kwa nini unaona haitomfikia? Mimi naamini jinsi matumizi ya ICT yanavyokua ndivyo watu wengi wananufaika na hizo huduma. Kwa hiyo unataka wahamishe wapeleke nchi nyingine? Watanzania bana, kitu kikiletwa kwenu hampendi, kikienda kwa jirani pia hampendi, sasa mwatakani? Ndio wale nyie akina kioze kitupwe, maana wewe hutumii na kumpa muhitaji pia hutaki, hizo roho zenu sijui zimeathiriwa na nini?