Tanzania: The Whistleblower and Witness Protection Act, 2015; watoa taarifa watalindwa kweli?

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Kwanza, nakumbuka mwaka 2011 Hoseah alituahidi kuja na Sheria ya Kulinda watoa Taarifa; lakini katika chungulia yangu nikashangaa kidogo (kwakuwa si mtaalamu wa masuala ya sheria) kuwa Tafsiri ya Kiswahili haijaakisi kilicho kwenye sheria ya Kiingereza.

Tunaitunga sheria hii kwa maslahi ya Watanzania au kuridhisha wahisani?

Na, imekuja kwenye public domain baada ya watu kulalamika kuwa Cybercrimes Act (Sheria ya Makosa ya Mtandao) haiwalindi Whistleblowers?

Wanasheria, tusaidieni kuweza kutufafanulia...

Wakuu EMT, Pasco na Nguruvi3, sijajua kama Mchambuzi naye yupo fit; tuwekeni sawa... Are we safe under this new law?

Natumaini kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaenda mbali zaidi, itakuwa na tovuti kama Whistleblower Protection Program (wengine wanaiita No Fear Act)

Meanwhile, nashauri wadau wasome attachment nyingine yenye uchambuzi wa kurasa mbili tu ya hali ilivyo kwa sasa.

Mkuu nngu007, thanks for your 2011 thread!
 

Attachments

  • Tanzania_Whistleblower_Bill.pdf
    333.6 KB · Views: 298
  • whistleblowing-laws-in-tanzania-120315.pdf
    69.7 KB · Views: 168
Last edited by a moderator:
Dar es Salaam,

ASHA-ROSE MIGIRO
15 th May, 2015

Minister for Constitutional and Legal Affairs
 
Is this a joke?

Procedures for making a disclosure
5.-(1) A disclosure may be made in writing, sign language or orally and may contain as far as practicable-
(a) the full name, address and occupation of a whistleblower;
(b) the nature of the wrongdoing in respect of which the disclosure is made;
(c) the person alleged to have committed, who is committing or is about to commit the wrongdoing;
(d) the time and place where the alleged wrongdoing is taking place, took place or is likely to take place; and
(e) the full name, address and description of a person who witnessed the commission of the wrongdoing if there is such a person;


Hawa jamaa wamekula maharage ya wapi?
 

Nadhani hapo kwa vile wametumia neno "may" basi haina shida maana yake sio lazima. So whistleblower mwenyewe atapima kama kuna haja ya kutoa hiyo disclosure.
 
Mkuu Invisible,

Kwa sheria hii na ile ya makosa ya mtndao ‘hatupo salama hata kidogo''

Sheria ya ''mpiga filimbi au mtonyaji'' ni mwendelezo wa ileya makosa ya mtandao kiaina

Sheria ya mtandao (inabidi kuficha jina) mbunge mmoja alinukuliwa na gazeti moja akisema kifungu 7(2b) mpokeaji wa ujumbe unaotajwa na sheria kama jinai, anaweza kushtakiwa.

Na mtoa huduma wa mtandao analazimika kutoa taarifa serikalini kwa lazima pale itakapohitajika).


Kifungua 8(sheria ya mtandao) kinasema ni makosa kutoa taarifa za siri hata kama ni za kuisaidia nchi( mfano matumizi mabaya ya maliza umma)

Kwa ufupi, sheria imewabana watoa taarifa ‘whistleblower' na wasambaza habari ‘main stream media ' na mitandao ya jamii.

Wengi wanadhani sheria ya makosa ya mitandao ililenga kuwalinda wananchi kutokana na uhalifu.

Ukiisoma kwa undani lengo lilikuwa kuzuia habari ‘muhimu' kutoka.

Tunajua kazi nzuri iliyofanywa na mitandao katikakufichua maovu

Sheria ya whisleblower maana yake imelenga kuwalinda watoa taarifa.

Sheria inasema (3) A person receiving the disclosure in terms of subsection (2) shall atall times maintain confidentiality of the disclosure and the whistleblower

Subsection(2) inataja mamlaka ‘competent authority'ambazo mtonyaji anaweza kufikishahabari.

Kwa maana nyingine tuhuma zipelekwe katika authority kama Polisi, PCCB Usalama wa taifa n.k.

Tumeona competent authority za nchi yetu zikiwakimya uhalifu ukifanyika. Nyingine zimetumika kuficha uhalifu.

Tunakumbuka baada ya whistleblower taarifa ya PCCB kuhusu Richmond ilificha ukweli.

Ndicho chanzo cha kuundwa kamati. Swali, mtonyaji alisaidia vipi kutoa habari kwa competent authority kama si kujiweka katikamazingira hatarishi?

Soma kifungu 6 (matter exempted..) kuna kufuli limewekwa kuhusu taarifa mtonyaji anazoweza kuzitoa.

Zipo zinazohusu ‘masilahi ya taifa' na hata mahusiano ya nchi na mataifa.

Tunajua uhalifu mkubwaunausisha mataifa kama ilivyo kwa balozi zilizohusishwa na mambo kadhaa hata mapesa yalipofichwa. Sheria hii ya utonyaji ina tija gani?

Sheria ya mtandao inatamka ulazima wa serikalikupata habari kwa lazima kutoka chanzo inachotaka.

Sheria ya mtonyaji inasema lazima atoe identity zake ikiwemo kazi. Inataka hata shahidi atoe id zake.

Utamlinda vipi mtonyaji ikiwa tayari kuna sharia inayotoa ulazima wa vyanzo kama mitandao kuwatajwa wahusika?

Yapo mengi ya kuongelea, ninachoweza kusema ni kuwa mswada huo hauna masilahi, whistleblower imewekwa makusudi ili kupunguza hasira dhidi ya mswada wa sheria ya habari unaopingwa

Muhimu, kwanini sheria hizi zinawekwa sasa hivi?

Kwanini serikali izuie uhuru wa habari kwa mkono wa kulia halafu itoe uhuru wahabari kwa mkono wa kushoto?
Hapa kuna nini?

Lengo si whistleblower, bali kuhakikisha ile sharia ya kulazimisha kuungana na TBC katika prime time inatimia kuelekea uchaguzi mkuu ili Kudhibiti habari kwa vyombo vya habari na watonyaji

Sheria ya watonyaji na ile ya mtandao ikiunganishwana ya habari, zinaua uhuru wa habari wa mtu, watu, taasisi na nchi.

Watoa taarifa hawatalindwa, na vyombo husika vimepewa mamlaka ya ku ‘contain' habari

Katika nchi ambayo vyombo vya umma vipo chini ya mtu au kikundi cha watu(siyo independent) whistleblower hatalindwa Zaidi ya kuwekwa katika mazingira magumu

Hatuhitaji sheria ya whistleblower tunahitaji uhuru wa kutoa na kupokea habari
 

Hapo kifungu kimetumia neno MAY,ina maana it is option kwa muhusika kutoa baadhi ya mambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…