Hizo ndo jezi ambazo watu wanazilalamikia? Mbona sioni ubaya wake.. Wanaozilalamikia walitaka ziwe za aina gani? Ingawaje hazina rangi zote 4 za bendera ya taifa, zipo poa sio mbaya sana wala sio nzuri. Kitu kingine wachezaji wanaonekana wamepanda au ni ufundi wa kamera? Kidogo niseme naangalia timu moja toka Afrika Magharibi. Miaka yote nimezowea kuona wachezaji wetu wana maumbile ya lishe la Unga-robo usicheze mbali hapa wanaonekana kila mtu at least kala na kushiba. Hii nzuri sana.