Ndugu wana Jukwaa la siasa naomba kutoa maoni yangu kuhusu siasa za upinzani nchini.
Wananchi wa Tanzania tangu siasa za upinzani mwaka 1992 ziasisiwe wamekua na ushabiki wa maneno na wa rohoni tu hawajashiriki actively kujiorganise na kusupport kile wanachokiamini mfano Kipindi cha Lyatonga Mrema
Kipindi cha Professor Lipumba.. yani wakiuwasha moto leo wakapigwa mabomu kesho ziiii kimyaa.
Zanzibar nako kadhalika, kupoa kwao huku kumesababisha yafuatayo:-
1. Kuwavunja moyo viongozi wao kwani kiongoz anategemea kuna nguvu ya wananchi nyuma yake lakini akipata madhila ya kufungwa, kutekwa au vyovyote alitegemea negative reaction isiyopoa itakayolazimisha watawala kusalimu amri kinyume chake hawa viongozi wanakamatwa kama makondoo na hakuna impact yoyote.
2. Wananchi wanaotegemewa ndio wanawategemea viongoz.. hii inachekesha yani mtu anategemea eti Mbowe ndio aandamane kumpa katiba mpya ukimuuliza wewe umefanya nn yy anatukana tu mitandaoni..
3. Kutegemea huruma ya dola yani mtu anakaa anategemea kuna siku serikali itaona huruma iwape wananchi kisa imechoka kutawala hilo jambo naamin halitatokea..
4. Kutokuweza kuiga mifano ya majirani wanaotuzunguka inaonekana reaction ya raia ndio inayoleta mabadiliko ya viongozi na katiba mfano Malawi, Kenya, Zambia n.k.
Yani siku tutaacha kukaa kuwalaumu na kuwalalamikia kina Mbowe, Lissu, Zitto tufahamu tuna jukumu la kuchukua hatua sis wenyewe ndipo tutapata tunachohitaji.
Leo watu wanamlaumu Mbowe kwa nn kazungumza na Mama.. Hebu tujiulize je tulimsaidiaje alipofungwa?
Tulionyesha reaction gani upinzani ulipokandamizwa? Au tumekaa kuwatukana tu wanapigwa risas tunaona kawaida wanauawa tunaona kawaida.
Mimi ningewasihi viongozi wa upinzani wa kweli watulie wavute mpunga wao kutoka serikalini hadi Watanzania watakapojitambua na kufahamu garama za kupigania haki.
Ni mawazo na maoni yangu tu.. naruhusu kutukanwa kusemwa vbaya na kila kitu.
Asanteni.