Bw. Ali Mfuruki kakosa cha kusema hali akijua kuwa ni lazima apate hiyo posho ya Mkutanoni. huwezi kuropoka tuu kuwa hatuajili Wa Tz kwa kuwa hawana ujuzi (skills) na serikali inalikubali hilo? Naomba tukumbuke kuna mtu mmoja aliwa kusema hivi,'Tuliweza kujipatia uhuru bila ya kukaribisha external skills na experiences, vile vile na kuongoza nchi kwa wakati ule'. Kama kuna biashara inafunguliwa sasa ya kusomesha skills nitaelewa, zaidi ya hapo ni wizi mtupu. Shuleni unajifunza theories na vitendo kidogo, Hivyo vinakusaidia kuendeleza ujuzi ulioupata shuleni. Je ni ujuzi gani wanaoutaka hao wawekezaji? Je, si, kuwasiliana, kuandika, kusoma, kusimamia wakati, nk? Je hayo wasomi wa TZ hawayajui? Ila wa nje? Ningemwelewa akisema uzoefu (Experience), lakini fresh from school atajua yote? je, haitaji kuongozwa na wenyeji kazini hata asimame mwenyewe? Acheni kutufanya wajinga. Je, ma-lecturers wetu wako wapi ? Hawaoni wanadharauliwa kwa kazi yao ngumu kwa watoto wetu? Je, hao wawekezaji ni nani anayezipitia bizinesi plani zao hapa Tz, ili kwamba tumweleze azirekebishe ziendane na elimu yetu wanaoiona duni, isipokuwa fedha yetu? Arise Tz arise.