Ninajua kuwa mnajua kuna serikali ya muungano na ile ya zanzibar. Lakini wabunge wetu bungeni kila wanapotoa mada utawasikia wanasema, na ninawanukuu...
huu ni umahiri wa serikali ya CCM
napenda kuipongeza serikali ya CCM
serikali ya CCm inajali matatizo ya wananchi wake
nk
mwisho wa kunukuu.
Hitimisho: kuna serikali ya muungano, serikali ya znz na serikali ya CCM, maana hata spika hajawi kumhoji mbunge hiyo serikali ya CCm iko wapi?
Yep, jibu liko wazi kuwa tunaserikali mbili tu. Zanzibar ni serikali inayoongozwa na CCM kwa kuwa na nyumba ndogo isiyo na maamuzi (CUF) wala ilani ya uchaguzi inayotekeleza. Hawajakosea !!! Ndugu yangu Zanzibar wanatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM
Kwa nini basi mbunge anaposimama bungeni Dodoma anasema naipongeza serikali ya CCM? Kwa nini asiseme kuwa anaipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwani kila mara tunahitaji kukumbushwa rais katoka chama gani? Unafiki huu utakwisha lini.....