Uzoefu unaonyesha sheria zinazoibana Serikali na sekta zake hazifuatwi kiumakini isipokuwa tu sekta hizo zikibinafsishwa ndio utaona mlolongo wa visheria kama vile hazikuwepo.Mfano kiwanda cha sigara kurazimishwa kuandika onyo katika pakiti za sigara pindi tu kilipo binafsishwa n.k.
Je na Tanesco iki binafsishwa kwa asilimia kama 80% ndipo utaona sheria na haki zote za mteja zinafuatwa.Lakini kwa sasa Tanesco wapo chini ya ubora lakini Tbs ipo kimya kabisa,huku kwetu Kijichi wiki na kitu sasa umeme unazima na kuwaka zaidi ya mara 30 kwa siku na tena Volt meter ilionyesha umeme walio urudisha mara kadhaa leo baada yakuzima na kuwasha ilikua ni Volt 100,ulipo rudi uliwaka dk.45 na kuzima tena hivi ninavyo tuma jamvini saa hii haujarudi.