Tangazo la el-shadai wapo fm

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,459
Reaction score
872,117
Hili tangazo lilikosolewa mno kwa kutumia lugha isiyo na ustaarabu, likarekebishwa lakini bado lina tatizo kubwa, limekosa uzalendo pale masanja mkandamizaji anaposema hakuna kitu cha bongo hapa! vyote vinatoka dubai ,uk na pakistan, kwahiyo sisi tunaohusudu na kupenda vitu vya bongo hatuna nafasi EL SHADAI SHOPPING COMPANY! jamani biashare zetu zisitufanye tukose uzalendo kiasi hiki, unaponda chako unasifia cha jirani loh
 


bado watu ni wajinga hawa hawana tofauti na wanauza twiga wetu nje kwa kukosa uzalendo kisa vijihela vdogo wanavyopewa,wanataka sifa kwa waarabu!
 
mkuu mambo ya biashara ukiyachunguza sana unaweza usiende hata shopping kwa hasira worry out hayo ni matangazo tu usiogope..
 
yanakera hata kama hatuna uzalendo na hatujui kutengeneza matangazo lakini ngrrrrrrr
 
Mbona matangazo kama hayo ni mengi tu. Hujasikia matangazo ya pombe yakituambia huu ndo urithi wetu? au mwanaume wa kweli hutumia dume condom! Kwa hiyo kama wewe hutumii kondom hiyo wewe si.......................!
 
Kama tangazo lina ukweli si tatizo.

Unategemea nini kama serikali umeua viwanda vyote Na vingine kufanya godown!

Kama hizo bidhaa wanatoa huko hawana sababu ya kudanganya kuwa zinatoka bongo
 
yanakera hata kama hatuna uzalendo na hatujui kutengeneza matangazo lakini ngrrrrrrr

Mnatakiwa kukerwa na serikali yenu iliyouza viwanda vyote na kugeuza magodown ya kuwekea mali za wachina.Mnataka watu watangaze bidhaa za bongo kwani zipo?!!acheni hizo!!!
 
Ni kweli hawana bidhaa za bongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…