Tanesco Mwanza badilikeni

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2012
Posts
1,986
Reaction score
3,151
Jumatatu ya wiki hii saa 6 machana baadhi ya maeneo ya malimbe-nyegezi umeme ulikatika, toka siku hiyo hadi muda huu haujawahikurudi, japo wahusika TANESCO wametaarifiwa sana.

Jna mida ya saa moja kasorobo binafsi niliwaona tanesco maeneo ya tatizo, nikajaribu kuwaomba wawezekutusaidia kwani tatizo limetuadhiri sana, wakaniambia wanashughulikia tatizo hilo, na kweli mida ya saa mbili walikuwa bado wanapanda kwenye nguzo na tochi kubaini chanzo cha tatizo.

Wakati napita karibu na gari yao niliwakuta watu 2, mmoja ni mfanyakazi wa tanesco na mwingine ni mtumishi wa hostel inayoitwa white house, mara nikasikia yule mtumishi wa hostel akimpatia yule wa tanesco sim aongee na mtu mwingine ambaye alikuwa hewani kwa wakati huo, yule mfanyakazi wa tanesco akasema "mzee si unajua lakin kubadilisha lain ya umeme ni kosa kisheria" akasogea pembeni wakaendelea kuongea.

Binafsi nilifikir kwamba tatizo lingeisha leo maana jana walianza jion sana, cha kushangaza ileo jioni ile hostel ya white house imepatiwa umeme bila shaka kwa kubadili lain wakituacha wengine giza totoro, sasa tanesco mwanza, ndo mchezo gani huo wa kifisadi kutaka kutuhudumia kimafungu, na tena hadi leo kimya hamjatuambia tatizo nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…