Maisha ni kuhangaika kila pahala na maskini wapo kila pahala katika dunia hii....
Kosa letu ni kudhani kuwa hakuna maskini weupe na kwa hivyo kila nchi ambayo kwa asili ina wenyeji weupe basi watu wake wote wana ahueni za maisha...si kweli, hizo picha ni ushahidi tosha.
Na kama mtu hatosheki na hizo picha basi na apite maeneo ya jamngwani karibu na klabu ya Yanga kwa wale walio Dsm, mtaona makundi ya maskini wa kihindi wakiishi kwenye nyumba zilizochoka na maisha yao ni ghetto style maana nyumba yenye wastani wa vyumba sita inaishi watu kama 30 hivi...you can imagine their level of poverty!