bado napitia pitia vyanzo vya habari na sioni tamko la Serikali
hivi waziri na naibu wake si wajiuzulu tu wenyewe maana mgomo huu ni kwa ajili yao!!
mpaka sasa kikwete yuko kimya
Heshima mbele wana jamvi
Ni zaidi ya saa 24 sasa tangu mgomo wa madaktari uanze.
Je, ni kweli serikali imeshatoa tamko au taarifa rasmi juu ya mgomo au bado. Na kama bado inasubiria nini. Au ndio uleule ugonjwa aliosema ndugu yetu mwingine ambaye naye yuko Ujerumani kwa ajili ya ‘check up' ya macho!? …yaani "Kutokuwa na Maamuzi".
Nimemuona jana Mh. Waziri Mkuu akiongea pale Ikulu lakini ilivyokuwa ni kama alikuwa anaongea kama Ngugu ‘Mizengo Pinda' na sio ‘Waziri Mkuu'. Nasema hivyo kwa maana iaelekea waandishi walimvamia na ndio akasema alivyosema kwa hiyo sidhani kama hiyo inaweza kuwa taarifa rasmi.
Nchi iko kwenye autodrive. Jk amejificha labda kafunga mungu ashuke. Alilia sana urais sasa afanye tuone. Wale wanaoutaka waone mfano wa kujipeleka huku una kichwa cha nazi
wako bize wanapanga mikoa mipya na wilaya mpya nani awe mkuu wa mko na wilaya kwani shangazi bado hajapata cheo, mjomba, kakabinamu, dadabinamu, mwanaasha naye ukuu wa wilaya ss akimaliza vyooooote hivyo ndipo aje kwenye suala lenu la madaktari na hapo inategema kama hajawa na kajisafari maana pasaka inakaribia shoping hatujafanya bado so endeleeni kusubiri tu tutakuja na majibu mazuri!!