junpyo
Member
- Feb 26, 2013
- 50
- 9
Utangulizi:
Awali ya yote tusimame dakika moja ya ukimya kuwakumbuka wahanga wa mauji yaliyofanywa na serikali kupitia vyombo vya dola Arusha tarehe 5 Januari 2011 wakati wa maandamano ya kudai haki pamoja na wote waliotangulia mbele ya haki mwaka 2011 mpaka 2012 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ajali, maafa na vifo vya kawaida vya viongozi na wananchi katika chamamwaka mpya.
Sekretariati ya chama imefanya maamuzi mbalimbali kuhusu masuala ya kiutendaji ya chama na kuandaa mapendekezo ya masuala mbalimbali ya kisera.
Aidha, Katika kuendelea kutekeleza maazimio ya kikao cha kamati kuu cha tarehe 20 Novemba 2011 chama kimefanya mabadiliko katika Kurugenzi ya Habari na Uenezi na kumteua John Mnyika kuwa Mkurugenzi, na kuwateua Erasto Tumbo kuwa Afisa Mwandamizi wa Kitengo cha Uenezi na Tumaini Makene kuwa Afisa Mwandamizi wa Kitengo cha Habari.
Sekretariati ya chama haijaridhishwa na mwelekeo wa taifa kisiasa, kiuchumi na kijamii katika mwaka 2011 na imeazimia kuitisha mkutano wa kamati kuu ya chama kuanzia tarehe 22 Januari 2012 ambapo pamoja na mambo mengine utapokea taarifa maalum ya hali ya siasa na kufanya maamuzi juu ya hatua za haraka za kusimamia uwajibikaji serikalini kwa maslahi ya umma kwenye mambo yafuatayo;
(i) Kipaumbele kikuu cha kisiasa cha taifa na chama kwa mwaka 2012 ni
kuboresha mchakato wa mabadiliko ya Katiba ili Tanzania iwe na Katiba mpya na bora.
(ii) Kipaumbele kikuu cha taifa na chama kiuchumi ni kunusuru uchumi wa nchi na kupunguza ongezeko la kupanda kwa gharama za maisha kwa wananchi na haswa mfumko wa bei na kuongeza uzalishaji.
(iii) Kipaumbele kikuu cha Kijamii ni kushughulikia vyanzo vya migogoro katika maeneo mbalimbali badala ya kukabiliana na matokeo haswa migogoro ya ardhi.
Mwelekeo wa Siasa:
Sekretariati ya chama haijaridhishwa na uwajibikaji katika serikali kwa umma ikiwa miaka minne imepita tangu kutolewa hadharani kwa Orodha ya Mafisadi (List of Shame) Septemba 15 mwaka 2007.
Chama kilitarajia kwamba mwaka 2011 ulikuwa wa kukamilisha uchunguzi na uchukuaji wa hatua dhidi ya wahusika katika kashfa mbalimbali ili kurejesha utamaduni wa uwajibikaji. Badala yake serikali imeendelea kuahirisha kuchukua hatua kamili serikalini, Bungeni na hata ndani ya chama chenyewe.
Katika kipindi cha mwaka 2011 pamejitokeza tena ufisadi mwingine katika ngazi mbalimbali na utamaduni umekuwa ni ule ule wa maazimio kupitishwa ikiwemo na Bunge bila utekelezaji wa haraka wa serikali na hatua stahiki za kinidhamu na kisheria kuchukuliwa kwa wahusika.
Katika Hotuba yake kwa Taifa tarehe 31 Disemba 2011 Rais Jakaya Kikwete hakuzungumzia hatua ambazo serikali yake imefikia katika kushughulikia mafisadi ikiwemo kuhusu hatua ambazo alipaswa kuchukua kufuatia maazimio ya Bunge. Hali hii ni kwamba, serikali na CCM imeelemewa na ufisadi na wameshindwa kuchukua hatua kwa kuwa ufisadi umejikita katika mfumo mzima unaowagusa pia viongozi waandamizi katika chama na serikali hivyo namna pekee ya kusimamia uwajibikaji ni kwa kuunganisha nguvu za wananchi katika kutetea rasilimali za taifa.
Aidha, kufuatia hatua za kisiasa na kijamii za chama na wadau za kuunganisha nguvu ya umma kwa njia mbalimbali; serikali ilikubali kuanzisha mchakato wa kufanya mabadiliko ya katiba. Izingatiwe kwamba katika Hotuba yake ya mwisho wa mwaka 2010 Rais Kikwete alitangaza kuunda tume bila sheria na hatimaye kufanya mabadiliko kwa kutumia vyombo vya kikatiba vya sasa. Baada ya msukumo wa CHADEMA na wadau wengine kutaka mchakato wa katiba uongozwe kwa sheria maalum itayoweka mfumo wa vyombo husika ndipo serikali ikakubali kupeleka muswada Bungeni.
Hata hivyo, haikuwa dhamira ya serikali toka mwanzo kuweka utaratibu bora wa kisheria wa kusimamia mchakato wa katiba mpya muswada huo uliwasilishwa kwa hati ya dharura, ukapingwa na kambi ya upinzani na wadau wengine, hatua iliyoisukuma serikali kuiondoa hati ya dharura lakini ikaendeleza hodhi ile ile katika upitishwaji wa muswada tarehe 18 Novemba 2011 na hatimaye kusainiwa na Rais tarehe 29 Novemba 2011.
Hatujaridhika na kauli ya Rais Kikwete "kuwa ndani ya robo ya kwanza ya mwaka ujao uundaji wa Tume ya Katiba utakuwa umekamilika" kwa kuwa kauli hiyo haisemi chochote kuhusu haja ya sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 kufanyiwa marekebisho makubwa kwenye Mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 31 Januari 2012 kabla ya vyombo vinavyohusika na mchakato wa katiba havijaanza kuundwa na kufanya kazi.
Tunahimiza chama nchi nzima kuendelea kutekeleza maazimio ya kamati kuu ya chama ya tarehe 20 Novemba 2011 kuhusu mchakato wa mabadiliko ya katiba na waraka namba 3 wa Katibu Mkuu wa chama kuhusu sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011. Tunahimiza viongozi wote wa chama na wa kuchaguliwa kupitia CHADEMA kuendelea kushirikiana na wadau kutoa elimu kwa umma kupitia mikutano na njia nyinginezo juu ya mapungufu ya sheria husika na haja ya mabadiliko kufanyika kabla ya vyombo kwa mujibu wa sheria kuanza kazi yake.
Mwelekeo wa Uchumi:
Tumesikitishwa na hali tete na mwelekeo mbovu wa uchumi wa nchi yetu na kupanda kwa gharama ya maisha kwa wananchi kunakoendelea kusababishwa na pamoja na mambo mengine mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya
shilingi.Hali hii sio tu ni tishio kwa maisha ya wananchi bali pia kwa usalama wa nchi kwa ujumla.
Na haswa ikizingatia kwamba Rais Kikwete hakueleza hatua thabiti na za haraka za serikali katika kukabiliana na hali hii kwenye hotuba yake tarehe 31 Disemba 2011. Badala yake ameendeleza utaratibu ule ule wa hotuba zake za kuorodhesha visingizio vya nje vya uchumi wa dunia bila kuweka mkazo katika kueleza hatua za kuinua uchumi wa ndani pamoja na kulinda wananchi dhidi ya misukosuko ya nje.
Pia, tunaitahadharisha serikali juu ya mkakati unaoendelea wa kukabiliana na hali hii kwa kuongeza malipo kwa baadhi ya viongozi waandamizi kama wabunge kukabiliana na ugumu wa maisha huku yenyewe serikali ikiikabili hali hiyo kwa kupandisha bei ya huduma za msingi zinazotolewa na taasisi zake huku ukimuacha mwananchi kwenye mazingira ya kipato kile kile wakati sekta ya umma ikiungana na sekta binafsi kupandisha bei za bidhaa na huduma. Hali hii ikiaachwa iendelee itakuza pengo la wenye nacho na wasionacho katika taifa na wakati huo huo itaongeza zaidi gharama za maisha kwa wananchi hususani wa kipato cha chini tofauti na ahadi ya Rais Kikwete na CCM ya kuleta maisha bora kwa kila mtanzania.
Aidha, Serikali ilipaswa kueleza ukweli wananchi kuhusu hali mbaya ya kifedha ambayo inalikabili taifa hivi sasa kwa kupungua kwa mapato ya ndani na ya nje ukilinganisha na bajeti iliyopitishwa na kufafanua mkakati wa kuongeza uzalishaji na kupunguza matumizi ya serikali.
Tutawasilisha taarifa maalum kuhusu mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa na chama pamoja na viongozi wa kuchaguliwa hususani wabunge ili kuweza kuzingatia masuala husika katika kazi za chama na za kuwakilisha wananchi.
Tunatarajia kwamba serikali ya CCM itazingatia mwito huu na kuwasilisha mpango maalum katika mkutano wa Bunge unaonza tarehe 31 Januari 2011 na kama sehemu ya utekelezaji wa mpango huo utafanya mapitio ya bajeti za Wizara zote za Serikali kwa kuzingatia maoni yaliyotolewa na Kambi ya Upinzani Bungeni. Pia, tunatarajia serikali kama ilivyofanya kwa suala la Katiba Mpya itazingatia hoja
toka kwenye ilani ya CHADEMA ya mwaka 2010 kuhusu hatua ambazo serikali inapaswa kuchukua katika kuinua uchumi wa nchi na kupunguza gharama za maisha kwa wananchi kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuongeza uzalishaji.
Mwelekeo wa Jamii:
Tumezingatia kwamba pamoja na ahadi za kila mwaka za serikali bado mwelekeo wa kuboresha huduma za msingi za kijamii hususani elimu, afya, maji na nyinginezo miaka 50 baada ya uhuru haulingani na umri wa taifa na rasilimali ambazo nchi inazo.
Aidha, tunatambua kwamba kuna ongezeko la migogoro ya kijamii katika taifa ambayo serikali badala ya kushughulikia vyanzo vya migogoro hiyo inashughulikia matokeo na hivyo kuendeleza migogoro zaidi.
Tumebaini kwamba mtizamo wa Serikali katika kushughulikia migogoro katika mwaka 2011 umesukumwa na maelezo ya Rais Kikwete ya mwishoni mwa mwaka 2010 kwamba: "Najua wapo baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa ambavyo vimepanga mikakati ya kuendeleza malumbano ya uchaguzi na kutaka Watanzania waishi kama vile nchi ipo kwenye kampeni za uchaguzi.Wamepanga wakati wote kutafuta jambo au hata kuzua jambo ili kuwachochea wananchi waichukie Serikali. Wamepanga kuchochea migomo vyuoni na maandamano ya wananchi mara kwa mara."
Katika hali hii madai ya haki za kisiasa, kiuchumi na kijamii ya raia na makundi mbalimbali ya kijamii yamekuwa yakishughulikiwa na Serikali na mara nyingine kwa maelekezo ya CCM kama vile ni msukumo wa CHADEMA na viongozi wake na hatimaye badala ya serikali kushughulikia madai ya msingi imekuwa ikiwashughulikia wanaotoa madai hayo au matokeo ya madai hayo badala vyanzo vya madai hayo.
Tunaitaka CCM, serikali na vyombo vya dola kubadilika kwenye mwaka 2012 ili kuepusha nchi kuingia katika malumbano na migogoro ya kijamii na badala yake watimize ahadi kuhusu huduma za jamii kama ambavyo waliahidi katika ilani yao ya uchaguzi.
Hatujaridhika na hatua za serikali katika kushughulikia migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, serikali na umma, na wananchi na wawekezaji katika maeneo mbalimbali yenye rasilimali za kilimo, misitu, madini na nyinginezo.
Chama Kimesikitishwa pia na namna ambavyo serikali inashughulikia matatizo ya wanafunzi na migomo katika Vyuo Vikuu na tumeagiza Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) kufuatilia kwa karibu hali hiyo na kuchukua hatua zinazostahili na kuwasilisha taarifa kwa chama kwa ajili ya hatua zaidi.
Hitimisho:
Tunatoa rai kwa umma watanzania na wanachama kutambua kwamba katika kusimamia vipaumbele vya kisiasa, kiuchumi na kijamii vya taifa na chama; CHADEMA kimejipanga kutimiza wajibu wa chama mbadala na chama kikuu cha upinzani nchini katika mwaka 2012 kwenye vyombo vya uwakilishi ambavyo tuna wajumbe wa kuchaguliwa na katika ngazi mbalimbali za chama.
Aidha, pamoja na kutumia mikutano ya maamuzi ya kiserikali na kichama tunawajulisha watanzania kwamba chama kitaendelea kutumia pia njia nyingine zote za kidemokrasia ili kuunganisha umma katika kuwezesha uwajibikaji na kuchochea maendeleo.
Hivyo, wananchi watarajie CHADEMA kuendelea na ziara kuanzia mapema mwaka huu katika mikoa mbalimbali mijini na vijijini tukiweka kipaumbele kwa maeneo ambayo chama hakikufika kwa ukamilifu katika mwaka 2011 kwa mujibu wa ratiba itayotangazwa na kamati kuu ya chama. Aidha, tunaendelea na maandalizi kwa ajili ya ushiriki mzito wa chama katika chaguzi mbalimbali za marudio zilizojitokeza na zitakazoendelea kujitokeza katika ngazi mbalimbali.
Pia, pamoja na kuunganisha umma kuhamasisha demokrasia na maendeleo kwa maslahi ya taifa; mwaka 2012 ni mwaka wa kuanza kwa uchaguzi mkuu wa ndani ya chama kuanzia ngazi ya msingi, matawi na kuendelea mpaka uchaguzi wa ngazi
ya taifa utakapofanyika mwaka 2013 kwa ajili ya kujenga oganizesheni thabiti ya chama nchi nzima.
Hivyo, tunahimiza wanachama na wapenzi wa chama nchi nzima kuwasiliana na ngazi zao za chama kwa ajili ya kupata maelezo kuhusu waraka namba moja na namba mbili wa katibu mkuu wa mwaka 2011 kuhusu uchaguzi wa ndani ya chama ili kuweza kushiriki katika kutimiza wajibu huu muhimu kwa chama na kwa taifa.
Aidha, izingatie kuwa masuala mahususi ya kisekta kuhusu hali ya taifa kiuchumi, kisiasa na kijamii yataendelea kufanyiwa kazi na kurugenzi mbalimbali za chama kwa upande wa chama na mawaziri vivuli kwa upande wa hatua za kibunge na za kiserikali.
Nimalize kwa kuwatakia heri ya mwaka 2012 na kuwaomba watanzania muendelee kuiunga mkono CHADEMA kwa hali na mali kwa mustakabali mwema wa taifa letu.
Dr. Wilbroad Slaa
Katibu Mkuu