Tafsiri: Wamachinga wanazunguka mitaani na biashara zao, hao wanaoondolewa na RC Makalla ni Wajasiriamali

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,961
141,959
Kiukweli akina mama lishe, wakaanga chips, wauza mboga mboga, wauza supu za utumbo, wachoma vitumbua nk hawa siyo wamachinga bali ni wajasiliamali wadogo wanaotambuliwa na Ilani ya CCM na hata ile ya Chadema iliyoshindwa.

Wamachinga ni wale wachuuzi wanaozunguka mitaani na bidhaa mkononi.

Nataka kuweka kumbukumbu sawa tu!
 
Unaweza kuwa na hoja ila unapowashambulia wengine kwa misingi ya ubaguzi wa itikadi hata hoja yako inapoteza maana.
 
Kwahiyo TANESCO na TANROAD hawana nguvu wala usemi juu ya miundombinu yao mpaka wanasiasa waingilie kati wanavyopenda wao.
 
Tatizo sio wamachinga tatizo lipo kwa wanunuaji.

Watanzania wengi kama ni nguo utanunua kwasababu umeiona na imekupendezea japo hukuwa na mpango wa kununua. Hapo lazima maachinga akuletee barabarani.

Pia kwa nchi yetu kuzui machinga nikuwaonea kama viongozi wenyewe hawana ubunifu, maono, uwezo na utashi utegemee wanaoongozwa watakuwaje.

Viongozi wamekuwa wahanga wa siasa hata pale pasipo na siasa( hakuna mtu mnafiki kama mwanasiasa, waongo kama nini) wao wanachokiangalia ni pesa! Pesa!pesa na hata vyeo vyao ni ili apate pesa! pesa!😂😂

Wamachinga tunawaonea wajameni
Wamesoma wamekosa kazi kwa taaluma zao! ajira hakuna mmekata kuwaajiri! wamejiajiri bado hamjawatengenezea mazingira wezeshi pengine wajikwamue kimaisha! Ndio hao wamachinga.

Wengine wapo bize kuzurura et wanafanya video za utalii😂😂😂😂
Kweli rais unafanya mambo yanamna hiyo kweli. Tumekuchagua utengeneze video za utalii? .wajameni hii nisawa kweli..haaah! Hapana nasema hapana!

Machinga endeleeni kukaa huko barabarani tena ikiwezekana uzieni katikati na sehemu za pundamilia mpange bidhaa yenu hadi kwenye madaraja😂

Haiwezekani mfanywe madaraja ya watu wapumbavu wakivuka wanaanza kuwafokea.
 
Kiukweli akina mama lishe, wakaanga chips, wauza mboga mboga, wauza supu za utumbo, wachoma vitumbua nk hawa siyo wamachinga bali ni wajasiliamali wadogo wanaotambuliwa na Ilani ya CCM na hata ile ya Chadema iliyoshindwa.

Wamachinga ni wale wachuuzi wanaozunguka mitaani na bidhaa mkononi.

Nataka kuweka kumbukumbu sawa tu!
Mkuu, upo sahihi kabisa. Hivyo hawa Wajasiliamali kwa mujibu wa sheria na taratibu ni sharti wafuate taratibu za biashara: wawe na sehemu rasmi ya kufanyia biashara, awe na nyaraka zote halali za kufanyia biashara yake, alipe malipo yote yatokanayo na biashara yake. Aidha Serikali ni jukumu lake kuwa kagua na kujirizisha na ufanyaji wa biashara yake. Aidha kuna kundi la wafanyabiashara kama wa vipuri vya magari, viatu na nguo, masufuria na vikombe, pombe na maji nk. ndio waliojifanya WAMACHINGA na kuzagaa mitaani na barabarani kwa kukwepa tozo zitokanazo na biashara zao na matokeo yake sasa wamewaletea matatizo AKINA MAMA (bibi zetu, mama zetu, dada zetu,) ambao walikuwa wanajiuzia magenge yao ya nyanya, pilipili, nazi nk kwenye vibaraza vya nyumba na wao kujiunga nao kuuza sehemu zisizo rasmi na sasa wote wana athirika kwenye zoezi hili. Aidha garengi bubu nazo licha kuleta uchafuvi wa mazingira kwa maana hawana vyoo pia zinaleta usumbufu mkubwa wa kelele na mionzi ya moto ya kuchomelea kwa watoto mitaani.
 
Back
Top Bottom