Tafakuri ya leo

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,501
Reaction score
6,649
TAFAKURI YA LEO.
​
1. Ana umri wa miaka 68 na sasa amestaafu kazi.

2. Alifanya kazi kwa bidii maisha yake yote akalea mke na watoto wake vizuri tu.

3. Alijinyima raha za maisha kwa kulipa ada ya shule ghali na gharama za maisha kwa watoto wake hadi nje ya nchi.

4. Sasa watoto wamekua na wako vizuri kimaisha huko Ulaya na mke wake amehamia huko kuishi na watoto wake.

5. Sasa yuko peke yake nchini kwake. Mke na watoto wake hawamjali tena.

6. Sasa imebidi aanze tena upya maisha ya u bachelor uku akipambana na shinikizo la damu na magonjwa mengine ya uzeeni.

7. Huu ndio ukweli kwa wanaume wengi wa tabaka la wafanyakazi wenye mke mmoja.
Uzee wao kwa kawaida ni wa upweke,shida na huzuni.

8. Wanawake wanapenda sana watoto wao zaidi ya waume zao...haijalishi mwanaume alipambana kiasi gani.
Kadiri anavyozidi kuwa mzee, ndivyo uthamani wake unavyopungua kwa mke wake.

9. Wanaume wanajitolea sana lakini wanaopata kuthaminiwa ni wachache sana.
😭😭😭😭
 
Na nyakati hizi ni ngumu zaidi kwa sababu,
Zamani kidogo watu walioana kwa sbb ya upendo kati yao.
Sasa hivi watu wanaingia kwenye ndoa wa sababu za uchumi, uchumi hakuna ndoa hakuna
 
Na nyakati hizi ni ngumu zaidi kwa sababu,
Zamani kidogo watu walioana kwa sbb ya upendo kati yao.
Sasa hivi watu wanaingia kwenye ndoa wa sababu za uchumi, uchumi hakuna ndoa hakuna
So wamefanya ndoa ni ajira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…