Exaud J. Makyao
JF-Expert Member
- Nov 30, 2008
- 1,518
- 25
Toa mchanganuo wa nini cha kufanya.Kwani kila siku Mama ntilie na machinga wanasumbuliwa,biashara ndogondogo zimevamiwa na wageni,ukianzisha mradi mkopo ni tabu na kodi lukuki,ebu tuelimishe basi nini kinaweza kututoa.
Amini kwamba inawezekana uishi maisha ambayo ni mazuri tena ya kukuridhisha wewe na wengine hapa hapa duniani.
Kisha fanya bidii kwa vitendo sawa sawa na imani hiyo.
Ejm
Ndugu yangu Mmaroroi, soma hizo bolds, ukiweka kichwani kuwa inawezekana, utaweza hata kwa kuanzia chini, sio lazima mkopo tu save taratibu na uwekeze hatua kwa hatua inawezekana tu. Kwani kina Peacock walikua na ajira, elimu, mikopo mikubwa? na wengineo walioanzia chini.
Jaribu pia kufanya vitu kwa kufuata sheria anzia na biashara ndogo, huku umeajiriwa, mikopo pia inapatikana kwa biashara ndogo mf Grocery, duka, nyumba zenye hati hata za kata wanapokea, mifugo: kuku, ngo'mbe.
Ukiwa na positive attitude utafanikiwa lakini ukikazania kuwa haiwezekani ndo basi tena. Mie nilikimbizia hiyo mikopo wee, nimeacha, sasa hivi nimeanza mifugo yangu itoshe matumizi yangu ya mwezi, then matumizi + fees ya mtoto, then matumizi + fees yangu + ya mtoto = Nisiwe tegemezi tena kwa mshahara ili niwekeze kwenye vitu vingine.
BADILIKA
Mama JOE,
Moja kati ya vikwazo vingi vinavyowazuia watu wasiendelee, ni kujifunza tu kwa WALIOSHINDWA, na kusahau kujifunza kwa WALIOFANIKIWA.
Kubadilika ni muhimu.
Toa mchanganuo wa nini cha kufanya.Kwani kila siku Mama ntilie na machinga wanasumbuliwa,biashara ndogondogo zimevamiwa na wageni,ukianzisha mradi mkopo ni tabu na kodi lukuki,ebu tuelimishe basi nini kinaweza kututoa.
Bidii bila maarifa ni kazi bure. Kwanza pata maarifa sina maana ya elimu ya darasani tu lah hata jinsi ya ku influence decision zinazofanywa na hao wasumbufu ni maarifa. ;;;;;;;;;;;;;;;;Acha confrotations toa suggestions/suppositions kwa kutumia hekima na busara; fanya networkings tengeneza mazingira mazuri na kwa wengine pia waweze kufanikiwa then utaona matunda ya maneno ya mwandishi wa hii thread.
QUOTE]
FELISTER,
Karibu tena.
Mawazo yako yamejaa utajiri wa kutosha kwa yeyote anayekusudia kuyatafuta maendeo kwa dhati na uhalisi.
Hili ni wazo zuri.
Lakini tuamini kabla ya kuona kitakacho tu aminisha?
Exaud na wengine,
Nini tulichoona ili tuamini?
Emma, Kama unaamini kuwa unaweza kuwa na biashara, kazi nzuri, elimu utatumia kila fursa inayopita mbele yako, lakini ukiamini kuwa haiwezekani kufanya chochote hata fursa nzuri inaweza pita mbele yako au ukaletewa ukaikataa si huwezi - haiwezekani tu ndo imejaa kichwani mwako.
Ndo tunasema mkopo mkubwa wa duka kkoo, contenas za Dubai etc haupo lakini je mkopo wa kuanzia biashara nyingine si upo?
Kuna watu wameishia form 6 kisa hakupata scholarship kwenda nje, kwani hapa hamna vyuo?
Kuna watu wanasota mtaani na degree kisa hajaona kazi inayomfaa, afu anaomba nauli ya daladala?
Ukiamini kila opportunity utaifanyia kazi, even if as a stepping ladder to the next level, kwasababu utakuwa na vision yako ya maisha bora.
Halafu anasema na "Kisha fanya bidii kwa vitendo sawa sawa na imani hiyo"
Mie nimetoa mfano wa ninachofanya, nadhani Exaudi mwenyewe economist atatupa mifano zaidi, au wewe pia.