Taarifa Kwa umma

katavi1990

New Member
Joined
Jan 26, 2015
Posts
1
Reaction score
0
CHADEMA Tanga.

Nawaombeni sana watanzania tusifanye makosa tena tunapokwenda kwenye uchaguzi mkuu. Tuhakikishe kura zote vyama vya upinzani yaani UKAWA kwa sababu upinzani umeonesha dhamira ya dhati ya kuwatetea wananchi haki kushindwa.

Mimi napiga kura za hasira kwakuwa CCM wametutawala kwa miaka zaidi ya 53 na maendeleo yaliyopo hayafikii kiwango ambacho CCM imekaa madarakani. Tunahitaji viongozi makini kuongoza nchi hii.

Kwakuwa watanzania wote mliofuatilia bunge mtaona wabunge wa UKAWA ndio wazalendo wa nchi hii nawaomba tafadhari sana.

Naomba nitoe mfano mmoja tu, kwa hapa Tanga stand imepelekwa Kange. Na kama serikali ya CCM ingekuwa na huruma isingepeleka stand Kange kwakuwa bado kuna maeneo makubwa ya kuweka stand.

Barabara ya 12 hadi ya 13 ule mtaa ungefaa kupanua na stand ingekuwa kubwa ya kutosha lakini wamewatia gharama na usumbufu.

Kwa kushindwa kuwaonea huruma wananchi kwasababu kila mnachofanyiwa mnalalamika uchaguzi ukifika wanashinda pia walikuwa na uwezo wa kupeleka stand uwanja wa Sabasaba matokeo yake ule uwanja unasemekana ni wa CCM na wakati ulikuwa na eneo la maonesho ya Sabasaba na Nanenane.

Hiyo ni baadhi ya mfano tu ambayo ila mpiga kura ajiulize hivi chama hiki kina dhamira tena ya kuleta maendeleo.

Itaendelea kesho.
 
Hivi yule jamaa mchumia Tumbo aliyegombea Ubunge kwa ticket ya CHADEMA 2010 bado yupo kweli..!!? Maana namjua ni kinyonga sana..
 
Kiwango cha maendeleo baada yq chama kukaa madarakani muda fulani kinapimwa na nini?
 
Hivi yule jamaa mchumia Tumbo aliyegombea Ubunge kwa ticket ya CHADEMA 2010 bado yupo kweli..!!? Maana namjua ni kinyonga sana..
Kwa hiyo wote waliogombea Chadema na kpigwa chini ni wachumia tumbo? Cc: Fredi Mpendazoe.
 
Asamte kwa taarifa mkuu. Wenye hekima tumekuelewa.
UBARIKIWE SANA.
 
UKAWA tafadhali simamisheni mtu makini na anaekubalika kwa watanzania!! tumechoka na serikali ya ccm. kura yangu ipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…