Mkuu umeibua suala muimu, kukosekana kwa hizo helikopta ni kielelezo kizuri kinacho dhihirisha kwa upande mmoja ni kwakiwango gani vyombo vyetu havijajiandaa kukabiliana na matukio ya dharula; na kwa upande mwingine ni mwendelezo wa tabia ya watendaji wakuu serikalini kuwapuuza raia wakati wanapopata matatizo. Nitoe mfano, idadi ya wamerikani ni takribani watu 250 milioni, na watu hao wanatembea sana sehemu mbali mbali duniani. hata hivyo,muamerika yeyote, bila kujali nafsi yake katika jamii akipatikana na tatizo popote duniani, serikali yake itafanya kila njia kumsaidia. Kwetu sisi watanzania walioko huko nje wakipata shida yeyote hakuna anayewasaidia. wakati mwingine nashindwa kuelewa mantiki ya kuwa na pasi ya kusafiri ya Tanzania.