Swali fikirishi: Hizi wapinzani si walisema hostel za UDSM mbovu? Mbona......

Naanza kwa kusema upinzani wa ulimwengu wa Tatu unakuwa na maana gani?

Tuliaminishwa hostel za UDSM hazitamaliza hata mwaka zitakuwa zimeporomoka, lakin nashangaa unaenda mwaka wa tatu sasa na hakuna dalili zozote za kuharibika kwa majengo yale,

Nikakumbuka suala la Ndege za Bombadier kwamba moja imekufa injini na haitafanya kazi kamwe,

Nikakumbuka daraja la kigamboni kwamba litaua watu muda si mrefu,

Sasa nauliza hivi ni kwamba upinzani unakuwa unakosa ya kumkosoa Magufuli mpaka walete ya uongo?

Kwa kipindi hiki cha Magufuli mbona ya kumkosoa ni mengi tena kwa hoja thabiti bila kuudanganya Umma?

Nadhani upinzani tujitafakari

Hapa unamtetea Magufuli au unachafua wapinzani? Unasema wapinzani walisema hizo hostel za Magufuli hazitochukua muda zitabomoka ila sasa ni mwaka wa tatu hazijabomoka. Je Magu toka ameapishwa katimiza miaka mitatu? Mada kuhusu hayo majengo ilikuwa ni ubora au bei? Naona post yako iko kiupotoshaji zaidi; lakini tuna uwezo wa kuchambua pumba na mchele. Kazana ndio raha ya demokrasia unaweka na propaganda kidogo ili unogeshe upotoshaji, shida ni pale mnapotumia police kujibu hoja.
 
Menda pale upige picha kama wewe ni mwanaume wa kisukuma...hostel zetu bado hata kupiga ka picha mnatuzuia....hivi watz zaidi ya mil 50 tuko chini ya mshamba mmoja!!?
I see ! Kwani ni lazima ukapige picha pale hostel ! Ungependelea watanzania milion 50 wawe chini ya wajanja wangapi ? Very shallow minded !
 
Naanza kwa kusema upinzani wa ulimwengu wa Tatu unakuwa na maana gani?

Tuliaminishwa hostel za UDSM hazitamaliza hata mwaka zitakuwa zimeporomoka, lakin nashangaa unaenda mwaka wa tatu sasa na hakuna dalili zozote za kuharibika kwa majengo yale,

Nikakumbuka suala la Ndege za Bombadier kwamba moja imekufa injini na haitafanya kazi kamwe,

Nikakumbuka daraja la kigamboni kwamba litaua watu muda si mrefu,

Sasa nauliza hivi ni kwamba upinzani unakuwa unakosa ya kumkosoa Magufuli mpaka walete ya uongo?

Kwa kipindi hiki cha Magufuli mbona ya kumkosoa ni mengi tena kwa hoja thabiti bila kuudanganya Umma?

Nadhani upinzani tujitafakari
Upinzani umekuwa km mwanamke jirani mwenye wivu, mume akileta friji home anachungulia anasema aaah hilo halikai wiki limekufa, akileta subwoofer anachungulia anasema aaah hilo mwezi tu limeunguaa

Upinzani hauna weledi km zamani tulipokuwa tunaletewa skendo za wizi wa mabilioni na mafisadi serikalini na ishu za kutowajibika kwa watendaji serikalini, sahv ni vululu vululu
 
Back
Top Bottom