Mimi nadhani ingekuwa vizuri kulizungumzia japo kwenye kifungu kidogo, hili suala siyo dogo ndugu zangu linaweza likasumbua sanaRasimu ya katiba imetamka wazi kuwa selikali haina dini ila kila mtu anauhuru wa kuabudu anachokiamini. Hivyo kila mtu anauhuru wa kujichinjia kitoweo kama ilivyo sasa kwa kuwa atakuwa havunji sheria yeyote ya nchi hii.
Nina wasiwasi na uelewa wako , hukusoma lipo hapa, si o lazima kila jambo liwe clearly expresed, impliedly pia inaruhusiwa, uwavyotaka wewe iwe, katiba itakua na pages zaidi ya 600, haya soma hapa , ibara ya 31.
31.-(1) Kila mtu anao uhuru wa mawazo, imani na uchaguzikatika mambo ya imani ya dini na anao uhuru pia wa kubadilisha dini,imani yake au kutokuwa na imani na dini.(2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwani huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ili mradi asivunje sheria za nchi.(3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje yashughuli za mamlaka ya Serikali.(4) Hifadhi ya haki zilizotajwa katika Ibara hii itakuwa chini yataratibu zilizowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii yakidemokrasia kwa ajili ya usalama, amani, maadili na umoja wa jamii nawa kitaifa na vitasimamiwa kwa utaratibu ulioainishwa kwenye sheria zanchi.(5) Ni marufuku kwa mtu, kikundi au taasisi ya dini kutumia uhuruwa kutangaza dini kwa kukashifu imani na dini nyingine, kujenga chuki aukuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini.(6) Dini na imani ya dini haitatumika kwa namna yoyoteitakayowagawa wananchi, kuleta uhasama au kuharibu amani miongonimwa wananchi.(7) Neno "dini" kama lilivyotumika katika Ibara hii litatafsiriwakwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na manenomengine yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwakwa maana hiyo.
haya sasa kazi kwako kuelewa
Nina siku ya Tatu sasa naipitia Rasimu ya katiba yetu ili nione kama hili suala la haki ya kuchinja vitoweo limegusiwa kwa namna yeyote ile, maana naogopa isije katiba ikapita bila kugusia hii ishu alafu ikaacha watu wakiendelea kuvutana kwa kitu kidoogo, kiasi cha kuuana na mbaya zaidi kutokuwa na BASE ya kikatiba katika kusuruhisha pande husika.
Mimi nadhani ingekuwa vizuri kulizungumzia japo kwenye kifungu kidogo, hili suala siyo dogo ndugu zangu linaweza likasumbua sana
Limegusiwa kwenye Utangulizi, aya ya mwisho maneno ya mwisho kabisa. Maudhui yake ni kwamba Serikali haina dini. Pia soma Ibara ya 31 (1) - (7) utaona kama kuchinja sio issue ya Serikali. Ukitaka kula mbayuwayu ruksa.
NDUGU, unapendekeza AYA ZA kuchinja za KITABU chako cha DINI iingizwe kwenye katiba ya nchi??????????????? mmmmh kesho tutasikia wakristo nao wakitaka AYA zao ziingizwe kwenye katiba
Nimekupata ndugu yangu, ndiyo maana wakati wa kutoa maoni nilishauri Serikali ichukue jukumu la kuchinja liwe lake ili kuondoa mgongano.
REJEA RASIMU YA KATIBA MPYA UKURASA WA 2
Of course ni changa mtoto, Lakini wee kwa maoni yako unahisi yaliyozungumzwa katika RASIMU YA KATIBA MPYA UKURASA WA 2 yanaweza kutuondolea mivutano?serikali inaundwa na watu wa dini zote na wapagani ambao watalazikika kuchinja kiserikali lakini pia inasemekana serikali ni ya mfumo kristo itaaminika vipi kubeba jukumu la kuchinja kwa niaba ya waisilamu?
Hujanielewa ndugu yangu, mimi nilitoa maoni kwamba suala la kuchinjwa liwe chini ya Serikali ili kuondoa uwezekano wa makundi ya watu kuligombea na kuhatarisha Taifa, Posible suala la kuchinja siyo la Muungano ngoja nisubiri kwenye Katiba ya Tanganyika na nifuatilia Katiba ya upande wa pili inasemaje.