Jokajeusi
JF-Expert Member
- Jun 1, 2018
- 6,332
- 10,913
Habarini Wakuu!
Alijibwaga sofani kwa uchovu. Uso wake uliakisi hasira kali huku midomo yake ikiwa imepauka mithili ya mtu aliyekuwa amekula ubuyu wa dodoma. kichwa chake kilichokuwa kimesukwa mabutu alikiona kama zigo kutokana na mawazo mengi aliyokuwa nayo. Maisha kwake yalikosa maana na kugeuka kitendawili kilichokosa mteguaji. Hakujua ni nini hatma ya maisha yake. Mwangaza wa matumaini ulishazima katika mboni ya macho yake. Tayari alikuwa kama mwanajeshi aliyejisalimisha kwa adui asiyemuona. Maisha kwake yalikuwa adui asiyeonekana lakini atoaye kichapo kikali.
Aliiangalia picha iliyokuwa ukutani ambapo picha hiyo ilimuonyesha yeye na Mume wake. Aliamka akaisogelea na kuitazama kwa makini kama mtu aliyegundua jambo jipya. Machozi yalimtoka na kutengeneza vimifereji vidogo vidogo katika mashavu yake makavu yaliyofubaa. Huenda alikumbuka kipindi kile akiwa bado ni binti mdogo jinsi alivyokuwa ameumbika. Umbo lake lenye ukaribu kabisa na namba nane lilikuwa limeyeyuka mithili ya pesa za pensheni. Sura yake nzuri yenye macho madogo ya upole ilikuwa imepotea njia na kuingia katika kambi ya magaidi. Masikini Dotnata, maisha ndio hayo sasa.
Miaka mitatu nyuma familia yake ilikuwa inakula shushu, raha na bata katika viunga mbalimbali vya jiji kubwa katika nchi ya Tanzania. Ilikuwa ni familia yenye furaha na amani. Kwa nini isiwe na amani wakati kila walichokitaka walikipata kwa wakati. Dotnata alikuwa mwanamke aliyesifika katika mtaa alipokuwa akiishi kutokana na mavazi ya gharama na urembo aliokuwa anatumia. Ukiongezea na sura yake na alivyoumbika ungesema hakuna mwanamke aliyefikia hata nusu ya uzuri hapa duniani.
Wengi walipenda kujua ni mwanaume gani mwenye bahati aliyemuoa Dotnata. huenda hata wewe ungekuwa miongoni mwa wakereketwa hao. Basi hakuwa mwingine bali ni Mimi Joka jeusi. Kipindi hicho nilikuwa nafanya kazi wizara ya mambo ya ndani wakati Mke wangu Dotnata akiwa ni Daktari katika hospitali ya Muhimbili. Kutokana na wote tulikuwa wafanyakazi tena tunaopokea mamilioni ya fwedha ilitufanya tuishi maisha ambao watu wengi huenda watayaishai siku ya mwisho wakifufuliwa.
Mke wangu aliniheshimu sana kutokana na kuwa nilikuwa nimeenda shule. kingereza ndani ya nyumba ndio ilikuwa lugha ya mzaha kwani mambo ya msingi tuliyajadili kwa lugha ya kijerumani. Hii ilitosha kuelezea wageni walikuwa wakitutembelea kuwa nyumba yetu ni nyota tano dizaini ya kimataifa.
Tulitoana jasho nyakati za usiku katika mechi za uchi wote tukiibuka washindi zawadi tusijue apewe nani. Ilikuwa hafu hafu, bampa tu bampa, ado ado na mwendo wa halichachi. Staili za misonge na mgongo wa tembo zilifanya kitanda kipate shida na kutoa sauti ungedhani ni sauti ya wachina wa kariakoo. Dotnata alikuwa analia kwa hamasa akikunja uso na kupanua mdomo kwa uhondo wa hogo la chang'ombe. Kilio chake nilikifananisha na sauti za cynthia muigizaji wa holllywood.
Kimbembe kilifuata, zimwi liliikumba familia. Dudu washa liliifanya familia iwashwe na kujikuna kila pahala. Mambo yalienda mrama. Ndoto na taraja zetu zilienda kombo. Kweli kikiwepo kitumie. Na ikiwaka mulika ikizima papasa. Kwetu iliiwaka lakini badala ya kumulika kwenye mambo ya msingi tuliwekeze kwenye magari na nguo za kifahari.Sasa Majuto aligeuka Babu yangu japo hatukuwa na undugu kabisa. Mimi na mke wangu tulifukuzwa kazi katika Sakata la Vyeti Feki. Kumbe elimu zetu zilikuwa za magumashi wakati watu walituona tumesoma kwa Mtaala wa Cambiridge.
Baada ya kufukuzwa kazi sikujua hata Kijerumani kilipotelea wapi achilia mbali kingereza ambacho nilikiongea kwa tabu sana. Kiswahili nilizungumza kwenye ishu za mzaha mzaha lakini ishu za msingi nilipiga kibantu nikiwa na Dotnata. ndipo nikagundua kuwa wakati wa shida ndipo unakumbuka vitu vya nyumbani. Nyumba ikaanza kupikwa Nguluka na majani ya tembele wakati tulikuwa tunakula Sato na Sangara kutoka Mwanza kabisa. Looh!! kweli maisha hubadilika.
Njaa ikapiga hodi. Mwanzoni tulikataa kuikaribisha lakini ilitusisitiza sana. Ilianza kwa kunong'ona ikisema "naombeni niingie ndani" lakini tuliikatalia. Muda ulivyozidi kwenda ilipaza sauti hata majirani walisikia na kujua kuwa njaa imeingia nyumbani kwetu.
Palipo na njaa kuna mafarakano. Palipo na njaa kuna magomvi, kuna kulegezwa. Palipo Njaa kuna maradhi na mauti ndio jawabu la mwisho.
Dotnata akaanza kuchoka. Umbo lote likayeyuka kama mshumaa. Sura ikashuka chini ungedhani ni kabibi kazee kumbe hata hajafikisha miaka arobaini. Ama kweli chezea vitu vingine ila usicheze na tumbo. Tumaini lililobakia lilikuwa moja tuu. Faraha iliyobakia ilkuwa moja tuu ambayo ilikuwa ni kubanjuana hasa nyakati za usiku. Lakini njaa nayo haikuwa nyuma ilitia timu huko nako. Njaa ilinipiga kiasi nikaanza kupoteza nguvu za kiume. Nilikuwa napiga kabao kamoja kama hati ya dharua bungeni. Kabao kenyewe kalikuwa kadhaifu tena ilikuwa ni ndani ya dakika mbili kametoka ptsuuuu!! ptu!. Mke wangu nae hakuwa na hamu tena ya kufanya mapenzi. Zile Sauti za kitanda zilizokuwa zinatoka kipindi kile tukiwa tumeshiba sasa zilikuwa hazipo tena. Yani mechi ilikuwa kama mechi ya bata kwani ulikuwa unasikia tuu "hoo! hoo!". Ndio hivyo tena. Sina ujanja.
Njaa ndio sumu namba moja ndani ya ndoa.
Karibuni!