sasa ndugu yangu viongozi hao hao ambao hawana utashi wa kuandika hiyo katiba mpya ndiyo hao hao wameamua kuandika katiba hiyo kama wanavyotaka wao. Ukisema zoezi hilo lisitishwe sasa utakuwa unamwambia nani zaidi ya hao hao viongozi waliamua kuandika katiba kwa maslahi yao.
Cha msingi hapa ni kupiga kampeni ya kuwataka wananchi wa tanzania wapinge hili zoezi kwa njia ya kutokwenda kwenye mikutano ya kukusanya maoni itakayoitishwa na tume ya kuandika hiyo katiba. Na kama wananchi hatakwenda kutoa hayo maoni basi tuone watawala watafanya nini.
Lakini kama kuna wananchi watajitokeza hata kama ni wachache basi katiba itaandikwa tu kwa msingi kuwa kuna maoni yamekusanywa. Na huku ndiko tunakwenda, kutakuwa tu na watu wataende kutoa maoni hata kama kwa njia ya kulipwa. Si uliona wale vijana walivyojitokeza pale Karimjee Hall siku zile za kujadili muswaada. Kuna walisema walihimizwa kufanya hivyo na viongozi wa chama fulani ingawa wenyewe walikuwa hata hawajui maana ya kwenda pale.
Pia hiyo kura ya kupitisha hiyo katiba baada ya kuandikwa itahitaji zaidi ya 50% tu ya watu watakaopiga kura kutoka kwenye daftari la wapiga kura bara na zanzibar. Sasa hata kama wapiga kura wakaojitokeza watakuwa watu 1000 na kati hao 501 wakapiga kura ya ndiyo basi hiyo itakuwa ndiyo katiba mpya ya watanzania wote zaidi ya milioni 40.
Hivyo ndiyo sheria aliosaini rais Kikwete juzi inavyosema.[Ukiona mtu anakushauri upumbavu, na wewe unamusikiliza na kuukubari, atakuwa amekudhareu sana (JK Nyerere)]