Suala la maji, Dar es Salaam

adobe

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Posts
2,770
Reaction score
1,883
Rais wetu mpendwa, juzi tuliona umetoa mitambo ya kuchimba maji na mitambo mizito kabisa, Sasa muda huu maeneo mengi Dar hayana maji na mto Ruvu siyo tegemeo tena.

Nakuomba mama Mpenzi tuonee huruma, mfuko wa maafa utumike kwa hali hii ya dharura vifaa ya kuchimba ulivyogawa vitumike kuchimba maji sehemu zile ambazo hazina maji kabisa hata kama yana chumvi ni bora kuliko hali hii kwa sasa.

Huku Dar kuna watu wana visima vya kuchimba ndo msaada kwa baadhi ya watu kwa sasa ila ni gharama kumudu, sasa kwa kuwa mitambo ipo naomba sana Waziri mkuu atumie mfuko wa maafa kuchimba visima.

Nakuomba sana Mama
 
Mtaani kwetu maji yapo 24Hrs.

DAWASA kwa hii mitaa yetu mnafanya kazi nzuri.

Nashauri tuwe tunaangalia mitaa ya kununua viwanja.
 
Tatizo hata visima virefu watu wangeweza kuchimba kuisaidia serikali
Swala ni hizo kodi za hivyo visima na masheria kama yote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…