Mfadhaiko ni hali inayotokea wakati ubongo unapokabiliana na tatizo la mvurugiko wa akili na kujikuta ukishindwa kuendana na hali zingine zinazohitaji umakini kwa wakati mmoja.
Mambo kadhaa yanayopelekea mtu kupatwa na mfadhaiko (Stress),kwa uchache tu!
1.Kufiwa na mwenza
2.Kutalakiana
3.Kufungwa jela
4.Kudaiwa
5.Kufiwa na mmoja wa wanafamilia
6.Kuugua ama kupata ajari yenye kupelekea majeraha makubwa.
7.Ndoa
8.Kufukuzwa Kazi
9.Kustaafu bila kujiandaa
10.Kukataliwa
11.Kufeli mtihani
12.Kushindwa kumudu majukumu ya familia.
Ishara kadhaa za mfadhaiko
1.Kuumwa kichwa kila mara
2.Maumivu ya shingo, maumivu nyuma ya mgongo,misuli kujikaza
3.Kuwa na mashakamashaka, kizunguzungu na wasiwasi usioisha.
4.Kusikia sauti au mvumo katika masikio
5.Hasira za mara kwa mara
6.Kutokwa jasho pasipo kufanya kazi yoyote
7.Kufunga choo, kuharisha na kupoteza uwezo wa kujidhibiti
8.Kupaniki
9.Maumivu katika kifua na mapigo ya moyo kwenda mbio
10.Kukojoa mara kwa mara
11.Kupungua hamu ya tendo la ndoa na ufanisi hafifu
12.Kuongezeka kwa hamaki au pupa na kuchanganyikiwa
13.Majonzi na huzuni
14.Kukosa utulivu katika mawazo na maamuzi
15.Kuwa mgumu ama mzito katika kujifunza jambo jipya.
16.Kujisikia mpweke na usie na thamani.
17.Kupungua kujipenda na kuwa mchelewaji
18.Kuongezeka kwa fedhea na maangaiko ya akili.
19.Kukata tamaa
20.Kuhamaki na kujibu kwa nguvu nyingi hata katika mambo madogo madogo tu.
21.Kuongezeka kwa idadi ya ajali ndogo ndogo katika shughuli zako za kila siku (Bahati mbaya nyingi)
22.Kujitenga na jamii na kukaa peke yako
23.Kuongeza matumizi ya sigara, unywaji pombe au matumizi ya madawa ya kulevya.
24.Kupenda vitu vya kubahatisha bahatisha au kamali. (Biko, Tatu mzuka, Meridian bet nk)
Mwandishi Helen Keller aliwahi kusema
"Although the World is full of suffering it is also full of the overcoming of it " kwa tafsiri isiyo rasmi ni sawa na kusema "Japo kuwa ulimwengu una mahagaiko lakini kuna njia za kuepukana/kuzuia" kwa uchache tu!
Namna ya kuepukana na mfadhaiko(stress)
1.Orodhesha vile vyote unavyohisi vinakupa mfadhaiko (stress)
2.Zungumza na rafiki yako ama mtu yeyote anaeweza kukusikiliza,ukamuelewa na ukafanyia kazi ushauri wake(kama tu ushauri wake unatija bhasi utumie)
3.Kubari kwamba kuna mambo mengine huwezi kuyabadilisha.Huna sababu ya kuumiza kichwa kwa mambo usiyoweza kuyabadilisha. Ukikubari kufanya hivyo itakupa nafuu kubwa.
4.Hakikisha unafanya mambo machache unayoweza kuyamudu.
5.Mwisho,Muamini Mungu kuwa ndie anae endesha maisha yako.
[HASHTAG]#NikutakieTafakuriNjema[/HASHTAG]