Stieglers Gorge itamwaga maji Dar

elivina shambuni

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
461
Reaction score
295
Dar es Salaam, inakwenda kumaliza shida ya maji kutokana na uamuzi na ubunifu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka(DAWASA), Injinia Cyprian Luhemeja kunuia kuleta maji kutoka maporomoko ya Stieglers Gorge.

Uamuzi huo, ulitangazwa juzi na Injinia Luhemeja, na kusema mchakato huo, tayari mc umeanza ikiwemo kuunda timu ya wahandisi wa mradi kufanya usanifu ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa utekelezaji wake huku fedha zitakazotumika zikiwa ni za ndani
Kwa mujibu wa mtendaji huyo mkuu wa DAWASA, utekelezaji wa mradi huo mkubwa utasaidia kuondoa ukosefu wa maji safi na salama kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na maeneo ya mkoa wa Pwani na kuifanya Dar es Salaam kuwa salama zaidi kwa matumizi ya maji safi na salama.

“ Kuleta maji kutoka kwenye maporomoko ya Stiegler’s Gorge ni muhimu na malengo yetu kabla ya Rais Dk. John Magufuli hajamaliza muda wake suala hili liwe limekamilika na yeye aweze kuzindua,” alisema.

Aliongeza lengo la kufanya hivyo ni kuboresha utoaji wa huduma za maji kwa kuhakikisha wakazi wa jiji la Dar es Salaam na maeneo yote yanayohudumiwa na DAWASA yanapata maji safi na salama.

“Tumeshaunda timu ya wahandisi wa kitanzania kuanza na mradi huu na malengo yetu tuliyojiwekea kabla ya rais Dk. Magufuli hajatoka madarakani mradi huu uwe tayari na kuanza kutumika kwa wananchi na utatekelezwa kwa fedha zetu za ndani, na katika hili Mheshimiwa Waziri tunamuahidi lazima tulitekeleze,” alisema.

Injinia Luhemeja alisema amekuja na mipango mbalimbali lakini katika siku 100, amenuia kuboresha utoaji wa huduma, kupandisha mapato na kusimamia miradi mbalimbali ya maji, ambayo ilikuwa inafanyika au kusuasua ikiwemo mradi wa maji Kimbiji na miradi mingineyo.

“Tutafanya kazi hilo ndio suala kubwa zaidi, sisi pamoja na menejimenti mpya tumeshaanza kufanya kazi na ndio maana tumejipa malengo ndani ya kipindi cha siku 100 ili kuhakikisha maeneo yote ambayo hayana maji yaanze kupata maji ikiwemo Yombo, Gongo la Mboto na maeneo mengine,” alisema.

Aliongeza “Tutamaliza miradi yote kwa wakati na katika siku na tungeomba zaidi ifikapo Desemba 9, mwaka huu wakati nchi inasherehekea Uhuru, wakazi wa Dar es Salaam nao washeherekee Uhuru wa kutumia maji safi na salama kwa kuwa maji ni uhai na kichocheo kikubwa cha uchumi,”

Injinia Luhemeja, alisema kuanzia sasa watafanya usanifu wa miradi yote ya maji inayotekelezwa na DAWASA kuona ufanisi wake na kuchukua hatua ikiwemo kuhakikisha mradi wa maji wa wilaya ya Kisarawe una malizika kwa wakati na kuwa na ufanisi mkubwa ili kuondoa tatizo la majisafi na salama.

“Uchafu wa majitaka kwenye makazi ya watu, tunataka kuondoa ikiwemo kuhakikisha kunakuwa na bei safi ya huduma hiyo sio kila mtu anajiamulia. Tutanunua malori 20 kwa ajili ya biashara hii ili kila mwananchi awe na uhuru wa kutumia malori hayo ambayo yatakuwa nafuu,” alisema.

Aliongeza “Zawadi yetu kwa Rais Magufuli hadi kufikia Desemba 9, mwaka huu ni kukamilisha mradi wa maji wa Chalinze, usambazaji wa maji upande wa Goba, Tegeta na maeneo mengine yaliyo karibu,” alisema.

Pia alisema ndani ya siku 100 watafunga mita nyingi za malipo ya kabla na wataanza ujenzi wa matenki ya Pugu na kusanifu upya mradi wa visima vya Mpera.
“Ndani ya siku hizo pia tutaongeza mapato kutoka shilingi bilioni tisa hadi kufikia shilingi bilioni 12 na tutahakikisha tunapunguza upotevu wa maji,” alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA, Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange, alisema watahakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi mkubwa ili kuleta maendeleo kwa wakazi wa Dar es Salaam kwa kuwa na majisafi na salama pamoja na kuondoa na kero walizokuwa nazo wananchi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo, alisema kitendo cha kuunganishwa kitaokoa Sh bilioni 2.9 kila mwaka zilizokuwa zikipotea katika uendeshaji wa Dawasa na Dawasco.

Alisema fedha hizo zitakwenda kusaidia upatikanaji wa huduma ya maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

“Serikali iliamua kuunganisha Dawasa na Dawasco ili kupunguza matumizi na fedha hizi zitaimarisha miundombinu na kuboresha huduma za maji katika eneo la huduma,” alisema.

Pia aliwaonya wafanyakazi wa Dawasa mpya kuacha tabia ya dharau, nyodo, kukumbatia matatizo na kuomba rushwa kwa wateja.

“Baadhi yenu mmekuwa na nyodo, rushwa na kuridhika na mafanikio kidogo, tabia hizi zikome kuanzia sasa,” alisema.
Aliitaka Dawasa mpya kujiendesha kama kampuni binafsi inayolipwa na wananchi wa Dar es Salaam na si idara ya Serikali ili kuongeza makusanyo ya fedha.
“Niwaombe mpunguze upotevu wa maji ambao kwa sasa asilimia 47 ya maji yanayozalishwa na Dawasa yanapotea,” alisema.
 
Pamoja na kuzungukwa na vyanzo vya maji kila kona dar ila bado walikuwa na shida ya maji. Sipati picha tanzania ingekuwa jangwani(sahara/karahali)
 
Sijaelewa maji ya bonde LA stiggilers Gorge yanaletwaje Dar? Moja huu mradi si uko hukoo porini Selous sasa maji yanaletwaje Dar? Au kachomekea neno stiggilers kuifanya habari inoge?
 
Kwahiyo mradi wa Bwawa la Kidunda umeota mbawa kama Gesi ya Msimbati au? Hii mambo ya kila kiongozi mpya kuja na vision yake inaleta shida sana.
 
Reactions: Auz
Kwa hiyo kila mkoa una dawasa yake, ambayo ina bodi ya wakurugenzi n.k. au ni upendeleo maalum kwa Dar Es Salaam?
 
Ule mradi wa visima vikubwa kule Kigamboni ulikuwa unapeleka maji wapi waungwana?
 
Sijaelewa maji ya bonde LA stiggilers Gorge yanaletwaje Dar? Moja huu mradi si uko hukoo porini Selous sasa maji yanaletwaje Dar? Au kachomekea neno stiggilers kuifanya habari inoge?
yavunwa,kusafishwa na kusafirishwa
Kwani hata haya tunayotumia sasa si yanatoka Ruvu?
 
Ukishasikia mtendaji kapewa ofisi kisha anaanza kusema anafanya jambo fulani kumfurahisha rais jua hapo ni siasa tu. Na sasa hivi imekuwa ni kama fashion kila mtu anamtaja rais kwenye jambo. Ukiangalia tija ya hilo jambo huoni.
 
Hutaki maji yaletwe Dar?
Umeelewa nilichoandika lakini? Kuna mradi wa bwawa la Kidunda ambao pamoja na mambo mengine unakusudia kuhifadhi maji kwa ajili ya majisafi Dar. Watu walishahamishwa tangu katika awamu ya nne ili kupisha mradi huo. Ndio nauliza umekufa au maji hayo hayatatosha?
 
Sijaelewa maji ya bonde LA stiggilers Gorge yanaletwaje Dar? Moja huu mradi si uko hukoo porini Selous sasa maji yanaletwaje Dar? Au kachomekea neno stiggilers kuifanya habari inoge?
Mto Ruvu uko jirani zaidi na Stigglers gorge, niitarajia ingekuwa cheaper kutumia chanzo cha Ruvu halafu hiyo nyingine ikawa ni long term plan.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…