Mhe. Masele: Kiongozi Kijana TZ asiyeogopa lolote (CV Attached)

Mwanzoni nilidhani suala la Escrow limekaa kizushizushi kwa sababu kulikuwa na upotoshaji kwamba hakuna mgogoro kati ya TANESCO na IPTL isipokuwa kuna mgogoro kati ya wabia wawili wa IPTL(VIP Engineering and Marketing na Mechamar), nikaona Masele yuko sahihi kumkoromea balozi kumbe balozi alikuwa sahihi kwa >100% na Masele alikuwa deadly wrong kwa >100%, inawezekana Masele alikuwa hajui/anajua ukweli wa sakata la Escrow akawa anapambana na balozi kwa kutojua ukweli au kwa makusudi huku akijua ukweli kwamba kuna wizi umefanyika kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, baada ya kutokea yaliyotokea NAFUTA kauli yangu ya mwanzo kwamba Masele alikuwa sahihi baada ya kujua ukweli, ukali aliyouonyesha naibu waziri Masele kumkoromea balozi wa uingereza ulikuwa wa kuwatetea wezi wa fedha za uma
 
CV ndogo sana ni tofauti na mleta mada alivyoisema. Ila kama mleta mada ni std 7 hii CV kwake ni kubwa sana. Anyway sijaona kikubwa hata kimoja hapo
 
Viongozi wetu mara baada ya kuteuliwa inapaswa kwenda kozi ya DIPLOMASIA pia na SHERIA kwa ajili kuwapa msasa ya jinsi ya kujibu/kujenga hoja vinginevyo nchi hii tutatengeneza maadui dunia nzima juzi tu AG/JAJI WEREMA kawaudhi wabunge toka nchini ZANZIBAR, kasha Membe akarusha kombora RWANDA (na M23 yao) sasa Masele na Uingereza duuh! bado MALIMA na VATICAN

:A S wink::A S wink::A S wink::A S wink:
 
Mbunge huyu kijana aliwahi kuwa Naibu Waziri kama sikosei wizara mbili tofauti katika awamu iliyopita. Sakata lake na Mh Ndugai pamoja na lile linaondelea katika Bunge la Afrika limempaisha zaidi hasa kwa wale waliokuwa hatumjui vizuri. Pamoja na kuwa kijana lakini hana makeke kama baadhi ya viongozi au waliowahi kuwa mawaziri vijana nadhani wengi tunawajua.

Tunaomba mwenye CV yake aiweke hapa tumfahamu vizuri.
 
Nimeisoma hii cv hakuna sehemu kusomea accountant lakini alikuwa afisa mikopo nani... Na leo ni mwakilishi wa watu wa Shinyanga mjini...sijui ninakokwama ni wapi??!
 
jamani hii familia ya kikwete hii,chukueni ccm ila nchi ni ya kwetu wote,Stephen masele ni swahiba wa ridhiwani jamani kikwete na familia yako tuachieni shy mjini yetu,ohoooo tumechoka mbona mnaing'ang'ania hivi kuna nini huko mwataka kuiba?
Dada kumbe kitambo unamjua huyo kijana
 
Back
Top Bottom