Stamani kumuoa tena !

Mlupembe

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2014
Posts
446
Reaction score
217
Wana jamii yamenkuta mie , nna msichana ambaye nimezaa nae na tunaishi pamoja , mwezi dec ndo nimelipa mahari ili ndoa iwe mei mwaka huu , lakini mambo yangu yameenda mrama kila nifanyalo pesa inakuwa ngumu hadi wife to be ananunua mahitaji ya kula hom , me nkajua tunasaidiana cha balaa shem mdogo wa wife jana kantumia sms kanichamba kinoma eti namzeesha dadae , kwanza nimuache , me ----- nalelewa tu matusi kibao , cha ajabu wife nae kanuna , kanishak kwetu eti mie najinunisha bahati home walivoniuliza nkawaeleza wakamweleza makosa yake , so anaomba eti nimsamehe ila mi nn hasira nae mno mana mbona wakati nnazo hadi huyo mdogo wake alikuwa anakuja kwangu.. Sie wote ni watumishi sa hatuwezi kusaidiana kweli ? Ushauri plz nimbwage au nimsamehe ?
 
Naona bado mna ka uvulana na ka usichana.
 
sababu ya kumbwaga mi sijaiona hapo!
 
Mambo haya mbona ni madogo mnataka kufurahisha umma!!! Ndoa ni kuvumiliana pale inapowezekana hasa pale kipato kinaposhuka inabidi kuwe na mshikamano mkubwa sana. Mkeo anahitaji kufundwa!!!
 
serious?! this is too personal!!kama kweli umefikia hadi kuwa na akili ya kuoa naamini una akili ya kufikiria hilo na kuacha kumwaga mpunga hadharani
 
Muoe tu braza,hapo mlipofikia si pa kurud nyuma,hakuna mtu mkamilifu,tunatofautiana tu viwango vya udhaifu!
 
Ukitaka kumuona Mme mwenzio jaribu kumuacha mkeo.hahaa kisa cha mpemba twanga ppta.
 
Haujawa tayari kuingia kwenye taasisi ya ndoa,
 
Kwani aliyekuambia unamzeesha ni nani yeye mwenyewe au mdogo wake ambaye hana mchango wowote katika maisha yenu? yaani hilo ndo la kutaka kumuacha? kwani kosa lake liko wapi kwani si ananunua chakula ndani,kwani kuna siku umelala na njaa au umesikia anatoka na mtu mwingine? nakuona hauko siriasi yawezekana hata mahari uliyotoa umeshinikizwa jipange ndo uanaume huo au ulifikiri mwanaume ni kuwa na dusheee peke yake!
 

mkuu.. niliona uzi mmoja hapa enzi nikiwa learner,

maudhui yake yalikuwa kama ya ki-isha mashauzi vile ila yalikuwa vere vere important! jitoe akili.. mwambie!!

'' kama unaona namzeesha dadako, njoo uchukue nafasi wewe ''!! babake sijasema mimi!

tumia namba nyingine lakiniiiiii!!!!
 
Kawaida katika maisha, kuna wakati gemu inakataa kabisa, hadi unaona ulimwengu unakuelemea, lakini haina maana ndio umeshindwa/feli, kubali matokeo huku ukiwa unaendelea kusikilizia michongo yako

Shem mdogo asikutishe kwa maneno yake, unajua hata baadhi ya ndugu wapo hivyo, mambo yanapoharibika wanaona wewe kama hujatulia, kumbe hawajui ukiwa mpiganaji kuna siku mambo yanaweza kukataa, ila haina maana itakuwa milele, ni muda fulani halafu unarudi kwenye chati
 
Tatizo dogo hivi unataka kumwacha wife?,je ukikutana na changamoto za ukweli utafanyaje?,ebu kua tuone kama kweli upo tayali kuwa baba wa familia.










Tatizo dogo hivi unataka kumwacha mamawatoto wako kweli?,je ukikutana na changamoto za ukweli utafanyaje?,samehe wife endelea na mipango ya ndoa.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…