Job Ndugai, spika wa bunge la JMT aliwahi kulitangazia taifa na dunia kwamba ana faili Milembe. Bila mashaka yoyote nadhani alimaanisha kwamba yeye aliwahi kuugua kichaa yaani kuwa na matatizo ya akili, na kutibiwa katika hospitali hiyo ya Milembe inayotibu watu wenye matatizo hayo. Alinukuliwa akimwonya mbunge mmoja...."Usinichezee, mimi nina faili Milembe"
Kauli hii ya Ndugai kwa mtazamo wangu, sio ya kupuuza hata kidogo. Inapaswa kuchukuliwa kwa uzito wake. Ina maana kubwa na ujumbe mzito ndani yake.
Ni jambo lililo wazi kwamba mtu mwenye matatizo ya akili hapendi kukosolewa kwa anachofanya, atakasirika. Ukimwambia asibebe uchafu atakuona mbaya, ukimwambia asile jalalani mtakosana. Ndivyo walivyo. Job Ndugai ametengemeza bunge dhaifu sana. Ni katika utawala wake bunge lilizimwa kuruka moja kwa moja.
Wapinzani walifukuzwa sana bungeni. Miswada mingi ya dharura isiyo na tija kwa taifa ilipitishwa kama ile ya madini mwaka 2017, ambayo baada ya kuwa sheria ilibadilishwa tena 2019 na kurudishwa kama zamani. Yote haya ni chini ya Ndugai.
Sheria ya tozo za miamala imepitishwa kwenye bunge la Ndugai, tena yeye mwenyewe akikejeli wananchi kwamba wanaopinga watoe mbadala. Yapo madudu mengi sana kwenye bunge la Ndugai lililopita na hili. Baada ya kujua kuna mdudu mengi anayabariki kufanyika, Ndugai akafanya mpango wa kujiwekea kinga ya kutokushitakiwa.
Cha ajabu sasa Ndugai hataki kukosolewa. Anataka kuwa juu ya kila mtu. Anataka kujifanya mungumtu. Hataki kusikia akiambiwa udhaifu wa bunge. Anatisha kila anayemkosoa.
Alipokuwa anajipendekeza kwa rais Magufuli katika mpango wa kubadili katiba na kumfanya Magufuli atawale milele, alisema Magufuli APENDE ASIPENDE ATALAZIMISHWA ili akubali kutawala milele.
Nadhani huyu Ndugai ashauriwe. Na ikiwezekana hayo matatizo yake ya akili yatazamwe. Faili lake alilosema analo liangaliwe vizuri ili kuona kama alimaliza tiba au anaendelea nayo.
Kiongozi wa mhimili mkubwa kama bunge ni hatari sana kuwa na matatizo ya akili, inawezekana ndio maana aliwahi kumpiga mgombea mwenzake kwa gongo wakati wa kura za maoni ndani ya chama chao.
Mwigamba Muchimati
Kisiwa cha Kwilela, Majita.