Speech ya Magufuli

Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Huyu Mzee kaifanyia nchi mambo mengi tu mazuri ambayo Watanzania wengi wanafahamu ukilinganisha na viongozi wengine waliowahi kupitia Wizara alizopitia yeye. Hivyo nafikiri unapotaka kuyasema mapungufu yake, kumbuka pia kuyasema mengi mazuri yake.
 

Kabisa huyu kwa maamuz anafanana na EL na ndo kiongOz anatakiwa awe na sifa hiz na kusimamia fact. Kma huwez kulipa Tsh 200 ogelea, hiyo ni fact tupu kwamba kwa gharama za uendeshaji kulipa Tsh200 bado ni gharama ndogo. Ukienda nch za watu pamoja wameendelea ila vitu vya umma bado bei zake ukiziweka kwa hela za Kitanzania ni hela nyingi. Hivyo Magufuli naona anafaa zaidi kuliko hata Membe
 
Ni kweli speech yake kwa wale tuliozoea zile za kuandaliwa na mtu mwingine ilikuwa 'substandard' lakini huyu mheshimiwa hata katika shughuli zake za kawaida ndivyo anaongeaga kimasihara hivi. Nadhani walioona press conference ya Obama pale Magogoni wanakumbuka aibu iliyotukuta kama nchi!
Kwa vile wengi tumeshawaza kimsingi kuwa tunataka 'rais dikiteta' na madikteta huwa hawajui kuongea bali kutenda, huyu ni 'semi-dikteta' na hatakaa na ngonjera bali uhalisia wa mambo. Kumbuka amesoma tangia ngazi ya sekondari hadi PhD na masomo yake ni Chemistry na Hesabu, hakuna cha ngini za kukaririsha hapo.
 
Hapana magufuli ataendelea kungozwa na kikwete kama remote kwaiyo tusifikirie mabadiliko kwa kuweka ccm tena..watanzania tusihadaike jamani hii nchi si yao peke yao..'
 

Umesema Kweli ila alikuwa anapeleka Maendeleo Chato. Ndo ilivyo. Lazima ufikrie kwako ndo wafuate wengine. Akiwa raisi chato utaipenda. Na bado yuko center
 

Magufuli ni mtu mzuri kuongoza nchi na ushauri wangu awe pm kidogo...mchaka mchaka wake ni wa uditekta... I am sure akiingia watumishi wa serikali wayaonyoola kazini saa kumi na moja asubui watakuwa kazini ila tunataka raisi msikivu kwa wanaachi kama lowassa na wengine
 
Huyu jamaa ana makumpuni ya ujenzi ya barabara zake binafsi ambazo zinapendelewa sana kwenye tenda.la pili anasumbua sana wakandarasi kwa kuwaomba ten percent.huyu ni fisadi mkubwa
 
Kiongozi umechelewa Na wewe ni mnafiki. Kama upo fair una andika mabaya Na mazuri ili tulinganishe.
upende usipende uchapakazi wa makufuli umechangia maendeleo makumbwa kwa nchi hii hasa Mikoa ya pembezoni.
shida yenu mkiishi Dar mnafikiri tanzania yote ipo hivyo.
ushindwe na ulegee!
 
Huyu jamaa ana makumpuni ya ujenzi ya barabara zake binafsi ambazo zinapendelewa sana kwenye tenda.la pili anasumbua sana wakandarasi kwa kuwaomba ten percent.huyu ni fisadi mkubwa

kwani jamaa wameshamchagua???? kiongozi gani ccm ana sifa za kuwa raisi ambaye sio fisadi au ambaye hajawah kukumbwa na kashifa za ufisadi???
wakimchagua magufuri itakuwa powaaaaa.. hakuna mtu aliyekamilika duniani..ongea na mazuri ya jamaa naamini 90% jamaa yupo safi na anafaaa kuwa raisi...
 
Huyu hawezi kuongoza nchi mana ana kichwa kilicho resi. Mtakuja kuniambia. Huyu anafaa tu awe mtendaji mfano waziri mkuu . Kumpa urais wa nchi ni utoto
 
Asithubutuuu...
 
huyu mheshmiwa ajifunze kutoa speech nzuri maana kashindwa kujieleza na hivi speech za mwisho wa mwezi ataziweza??!!!!

Jana haikuwa siku ya 'speech' Bali kuomba kura kwa wajumbe hivyo unatakiwa kuchagua nini cha kusema ndani ya dakika chache ulizopewa Jambo ambalo Magufuli ameliyanya tena kwa ufasaha Mkubwa kiasi cha wajumbe kushindwa kujizuia kumshangilia.

Kuhusu Speech za mwisho wa mwezi 1. Ni Utashi wa mtu na siyo za kikatiba
2. Kila 'speech' inategemea na mada (topic) kusudiwa , Magufuli mhadhiri mzoefu kutendea Haki mada ni Jambo la kawaida sana kwake. Labda humjui wewe Dr Magufuli vizuri au una sukumwa na chuki tu binafsi au za mgombea wako kukatwa au hofu za upinzani.
 

So what!!,Yan wewe kila kitu unakosoa,sisi binadam kila mtu na kasoro zake,kagombee wewe basi kama huna kasoro😡😡😡😡😡
 

Kiongozi mzuri yeyote ni lazima aige mfano wa Magufuli kiutendaj nw maamuz , jaman tuseme yoote hata kumchafua lkn Magufuli ni Rais bora awamu ya 5
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…