Tatizo kubwa au gonjwa kubwa duniani ni kutojijua au kumjua mbaya wako ni nani ktk ulimwengu huu tunaoishi.Kwanza kabisa tufahamu kwamba ni waandishi wachache wenye kuleta habari za ukweli na wengi hupendelea propaganda ambayo ndio iliyosababisha kwa Sudan kujigawa.Na wale wenye nguvu ndio wanaoweza kusambaza habari ambazo sio za ukweli bali unafik mtupu.Na hii ndio inayosababisha watu kuchukiana kwa kugombanishwa kwa makusudi ili wengine wafaidike.Na waafrika kama hawajaamka sasa hivi na kuungana na kulinda hizi rasilimali ambazo zinawafaidisha watu wa ulaya basi tutakaa kama wajinga na kugombanishwa na kupewa silaha mkononi halafu unaambiwa nenda kapigane na wale kwasababu sio dini yako au sio kabila yako.Haiwezekani nchi isiwe na maelewano kama mtu hajatia mdomo wake.Kwani hao magaidi wanapata silaha kutoka wapi?Hebu jiulizeni wenyewe.Mimi ninavojua silaha wanaosambaza ni wazungu ndio wenye kupenda kuona nchi inamwagika damu lakini huko kwao wanjilinda hata kama kunatofauti basi wanazimaliza kimyakimya.Na kwanini matatizo ya Afrika hayamalizwi na waafrika wenyewe mpaka waje wazungu ndio wasaidie kwa kishindo na kuua kama wanyama.Kwani kunafaida gani kuwepo na AU ikiwa wazungu ndio wakuleta amani.Kwanini hawajilindi wenyewe na jeshi lao na sisi tujilinde wenyewe na jeshi letu.Kuna maswali mengi ya kujiuliza kwasababu uchumi wa afrika ulitakiwa uwe juu na nchi zingeendelea lakini pamoja na rasilimali zilizokuwepo nchi ni masikini na tusubiri wazungu waje watusaidie kila mwaka kwani wao wanarasilimali gani kwenye ma nchi yao?Mbona barabara zao ni nzuri mahospitali yao ni mazuri elimu yao ni nzuri kwani huku tumekosa nini?Hii rasilimali tu iliyoko basi ilitakiwa kusomesha watoto bureee kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu.Kama alivokuwa anafanya Gadafi kwa watu wake maana walipewa kila kitu kasoro huo uhuru tu wa kumkosoa ndio walikuwa hawana.Na watajuta baadae maana nchi ilikuwa haina deni lakini sasa watauana kila siku huku wazungu wanajichotea mafuta vile watakavo.