South Africa election

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
362
Reaction score
909
AFRIKA KUSINI TAIFA LENYE HISTORIA AFRIKA, HIVI NDIVYO UCHAGUZI WAKE UNAVYO FANYIKA.

Na. Comred Mbwana Allyamtu.
Tuesday -7/5/2019.
Marangu, Kilimanjaro-Tanzania.


Kwa mujibu wa katiba ya Afrika kusini ya 1994, Kifungu cha 4, Sehemu ya 88 (Section 4 Cap 88) inaelekeza kwamba "Rais atachaguliwa na wabunge wa baraza la chini (National Assembly), kutoka Bunge la Afrika Kusini. Kwa kawaida rais hutokana na chama chenye majority vote/seats na huwa ni kiongozi wa chama kikubwa zaidi bungeni(kilichopata viti zaidi ya 201).

Rais wa kwanza kuchaguliwa chini ya katiba mpya alikuwa Nelson Mandela, katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia wa mwaka 1994, ambaye alifuatwa na Thabo Mbeki mwaka wa 1999 aliyetawala mpaka mwaka 2008 alipo jiuzuru kufatia mzozo wa kisiasa ndani ya chama chake cha ANC, kisha akafuatiwa na Kgalema Motlanthe mnamo Septemba 2008 na kisha Jacob Zuma mnamo Mei 2009. Kwa mujibu wa katiba ya Afrika kusini Kifungu cha 5, sehemu ya 88, ya katiba hiyo inasema "Rais atahudumu ofisini kwa mihula miwili ya miaka mitano tu". Nchini Afrika kusini Marais huchaguliwa ndani ya bunge, kila baada ya uchaguzi wa wabunge kumalizika, na baada ya rais kuchaguliwa hupewa muda wa miaka mitano, kwa mihura miwili.

Chini ya katiba ya mpito (ilokubaliwa kuanzia mwaka wa 1994 hadi 1996), kulikuwa na Serikali ya Muungano wa Taifa, ambapo mbunge kutoka chama cha upinzani atakayefata kwa kura nyingi waliweza kupewa nafasi kama Naibu wa Rais. Na hii ilitokea kwa rais wa mwisho wa nchi, hiyo kipindi cha utawala wa ubaguzi wa rangi F.W. De Klerk, aliwahi kuhudumu kama Naibu Rais, katika katika utawala wa Nelson Mandela kutokana na kuwa chama chake kupata idadi kubwa ya viti bugeni nyuma ya chama cha ANC na kukifanya chama chake cha AD kuwa chama kikubwa cha pili katika bunge jipya. Lakini De Klerk baadae alijiuzulu na kuendelea na upande wa upinzani na chama chake.

Uchaguzi Mkuu Afrika kusini kwa awamu hii utafanyika hapo kesho mnamo Mei 8, 2019, uchaguzi huu unafanyika kutafuta wabunge wa Bunge la Taifa (SOZA), na wabunge wa bunge la majimbo (NCOP) katika kila jimbo kati ya majimbo (Mikoa) tisa ya nchi hiyo.

Uchaguzi huu utakuwa ni uchaguzi wa sita kufanyika tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi mwaka 1994 nchini humo, na uchaguzi huu ndio utaamua nani atakuwa Rais wa Afrika Kusini.

Rais wa sasa Cyril Ramaphosa ataongoza chama chake cha African National Congress (ANC), chama kinachojaribu kutetea nafasi ya kubaki madarakani ili kuurejesha utawala wa Ramaphosa kwenye ikulu ya Union building iliyopo katika mji wa Pretoria, safari hii Ramaphosa anatetea nafasi yake ya awamu ya pili atakayo hudumu kwa muda kamili katika ofisi kama rais, Ramaphosa ni mrithi wa Jacob Zuma, ambaye alikuwa mtangulizi wake, Zuma ambae alijiuzulu kutoka ofisi ya raisi mapema tarehe 14 Februari 2018, kufatia mzozo ulioibuka ndani ya chama kutokana na madai ya tuhuma mbali mbali zilizokuwa zikimuandama Jacob Zuma.

Iwapo Ramaphosa atashinda uchaguzi huu atahudumu nafasi ya urais kwa kipindi kimoja tu kwa kuwa alikuwa tayari ameshahudumu kama rais halali kwa karibu miezi 12 toka alipo chukua madaraka hayo mnamo February 16/2018 kutoka kwa Jacob Zuma, hivyo hatoweza kugombea tena nafasi hiyo kwa awamu ya tatu katika ofisi ya uraisi, na hii ni kwamujibu wa Katiba ya Afrika Kusini Kifungu cha 6 Sehemu ya 88 (Section 6,Cap 88), ambayo inamtaka kuwa "Iwapo Rais yoyote atakae kaimu/atahudumu nafasi hiyo kwa miezi 12, kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika atahesabiwa kuwa amehudumu kipindi kizima cha muhura wake wa kwanza" ... Na kwa mashariti ya katiba ya nchi hiyo ni razima rais ahudumu awamu mbili ya miaka mitano mitano tu.

Ikumbukwe kuwa Afrika Kusini ni taifa linalotumia mfumo wa bunge (Parliamental system) katika kuundwa kwa serikali yake, Bunge la nchi hiyo (SOZA) linajumuisha jumla ya wabunge 400 wanaochaguliwa moja kwa moja na wananchi (direct vote) kwenda kuwa wawakilishi wa wananchi wa Afrika kusini.

Katika mfumo wa bunge nchini humo limegawanyika pande mbili katika kuundwa kwake, upande wa kwanza ni bunge linaundwa na Wabunge mia mbili (200) ambao huchaguliwa kutoka katika miji ya nchi hiyo na wengine 200 ambao wanachaguliwa kutoka katika mikoa (Majimbo) kati ya mikoa tisa ya nchi hiyo. Baada ya uchaguzi kumalizika na wabunge kupatikana ndipo Rais wa Afrika Kusini anachaguliwa na Bunge baada ya chama kitakacho ongoza kupata viti vingi vya wabunge vinavyohitajika kwenye Bunge ili kuunda serikali ambayo ni lazima chama hicho kifikishe viti 201 (Seats needed for a majority) ili kiteuwe rais atakae idhiniswa na bunge.

Katika Bunge la mkoa(NCOP), ambalo hutofautiana kwa ukubwa na bunge la taifa, pamoja na kupeleka wabunge Katika bunge la taifa kutoka kwenye mikoa ambayo huwa na wabunge 30 hadi 80, kutegemea na idadi ya kila mkoa katika kutoa wakilishi wa kawaida kutegemea idadi ya asilimia ya kila chama ilichopata.

Wawakilishi wa kila jimbo (Mkoa) watachaguliwa na bunge husika za mikoa huku baraza kuu la Taifa ya Mikoa (NCOP - National Council Of Provincial legislature) ina wajumbe 90, kumi kutoka mikoa yote tisa ya nchi hiyo, ambao wanachaguliwa na kila bunge la mkoa. Kikawaida Wabunge wa NCOP huwa wanachaguliwa na bunge za mikoa kulingana na idadi ya kura kwa kila chama kutokana na kiwango cha kura zilizopatikana kutoka mikoa husika.


Nje ya hayo uchaguzi huu kumekuwepo ya ongezeko la wapiga kura kwa asilimia 14% kutoka uchaguzi wa mwaka 2014. Kwamujibu wa tume ya uchaguzi ya EIC imesema kuwa wapiga kura wa mwaka huu ni milioni 27.1, huku Wapiga Kura wa ndani (Local Voters) wakiwa ni milioni 26.85 na Wapiga Kura wa nje (International Voters) wakiwa ni 179,334.

Katika uchaguzi huu karibu vyama 27 vime jisajili kushiriki katika uchaguzi huu ambao umekuwa na mivutano mikali hasa katika mambo ya aridhi (urudishwaji wa mashamba bila fidia), ajira, wimbi la wageni, usalama wa taifa, uchumi, miundombinu na mfumuko wa bei. Kila chama kilizindua kampeni zake ili kutafuta ungwaji mkono kwa wapiga kura wao. ANC ilizindua kampeni zake Katika mji wa Durban mahali ambapo ndipo ilipo hitimisha kampeni siku ya tarehe 5/5/2019. AD wao uzinduzi na utamatishaji wa kampeni zao ulifanyika Katika mkoa wa Western Cape Katika mji wa Cape Town mahali ambapo kina wafuasi wengi wanao waunga mkono.

EFF nao walifanya uzinduzi wao uliofanyika mkoa wa Kwazulu Natal katika mji wa Pretoria na kutamatisha kampeni kwenye jiji la kibiashara la Johhanesbug kwenye kitongoji cha Soweto katika uwanja wa Orlando Stadium. Kati ya wagombea wote 27 ni wagombea wanne wanaotazamwa kufanya vizuri katika kulitawala bunge la SOZA la Afrika kusini lilopo kitongoji cha Wiznbug Katika mji mkuu wa kibunge (legislative headquarter), wagombea hao ni pamoja na;

CYRIL RAMAPHOSA, Mgombea huyu anatoka chama tawala cha AFRICAN NATIONAL CONGRESS (ANC), alichukua madaraka ya uraisi mapema mwaka jana kutoka kwa mtangulizi wake Jacob Zuma. Uchaguzi uliopita wa 2014 chama chake kilipata asilimia 62.15% ya kura, viti vya ubunge ilipata viti 249, na Ndio Rais wa Afrika Kusini kwa sasa.

MMUSI MAIMANE, Mgombea huyu anatoka chama cha DEMOCRATIC ALLIANCE (DA). Uchaguzi uliopita chama chake kilipata Kura 22.23%, viti vya ubunge 89 hivyo anahitaji viti 112 kufikia viti 201 ili waongoze Bunge.

JULIUS MALEMA, Huyu anatoka chama cha ECONOMIC FREEDOM FIGHTERS (EFF). Uchaguzi uliopita alipata Kura 6.35%, viti vya ubunge 25 hivyo anahitaji viti 176 kufikia viti 201 walikamate Bunge.

MANGOSUTHU BUTHELEZI, huyu anatoka chama cha INKATHA FREEDOM PARTY (IFP). uchaguzi uliopita alipata Kura 2.40%, viti vya ubunge 10, anahitaji viti 191 kufikia 201ili aliweke Bunge kwenye himaya yake. Kiongozi huyu kinachomponza ni kuwakifu wapiga Kura baada ya kuongoza chama kwa Muda mrefu bila mafanikio ameanza kuingoza IFP tangu Tr. 21 Machi, 1975.

Afrika Kusini ni nchi yenye wakazi takriban milioni 56.72. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2016, Imepakana na Namibia,Botswana,Zimbabwe,Msumbiji na Uswazi.Nchi nzima ya Lesotho iko ndani ya eneo la Afrika Kusini. Mji mkubwa ni Johannesburg. Majukumu ya mji mkuu yamegawiwa kati ya miji mitatu:Cape Town ni makao ya Bunge,Pretoria ni makao ya Serikali na Bloemfontein ni makao ya Mahakama Kuu.


Chanzo cha Afrika Kusini kama nchi ni Koloni la Rasi iliyoundwa na Waholanzi katika eneo la Cape Town.Huko kabila jipya la Makaburu lilijitokeza kati ya walowezi Wazungu kutoka Uholanzi,Ufaransa na Ujerumani. Lugha yao ilikuwa Kiholanzi iliyoanza kuchukua maneno ya Kifaransa,Kiafrika na Kiingereza na kuendelea kuwa lugha ya pekee iliyo zaliwa na kuitwa Kiafrikaans.

Karne za kwanza za koloni la Kiholanzi zilishuhudia pia kufika kwa watumwa kutoka Indonesia walioletwa kama wafanyakazi wa Waholanzi na Makaburu.Hao Waindonesia walikuwa chanzo cha jumuiya ya Uislamu kwenye rasi ya tumaini jema (Cape of good hope). Pia machotara walitokea kutokana na kuzaliana kati ya Makaburu na wanawake Waafrika na Waindonesia.Sehemu ya machotara hao wameingia katika jumuiya ya Makaburu na wengi wao wanapimwa kuwa na mababu Waafrika.

Katika miaka ya baadaye ubaguzi wa rangi uliongezeka na watoto machotara wa Wazungu na Waafrika mara nyingi hawakukubalika,walianza kuishi kama kundi la pekee kati ya Waafrika na Wazungu,nao ni chanzo cha hao walio kuja kuitwa baadaye "Cape Coloreds". Sehemu kubwa ya eneo kaskazini kwa rasi ilikaliwa na makabila ya Waafrika.


Mnamo mwaka 1800 falme na milki zilianza kutokea hapa.Mwanzo wa karne ya 19, Wazulu chini ya Shaka Zulu walioanza kuenea na kuwashambulia majirani katika vita vya Mfecane. Vita hivyo vilileta uharibifu mkubwa lakini vilisababisha pia kutokea kwa milki za Wasotho na Watswana na wengine walioiga mitindo ya Wazulu na kujenga madola yenye uwezo wa kijeshi kama ilivyo kuwa kwa wazuku.


Mwaka 1814 Koloni la Rasi lilitwaliwa na Waingereza na kuwa sehemu ya Milki ya Uingereza. Utawala wa Waingereza ulisababisha uhamisho wa nje wa sehemu ya Makaburu waliotokana na Wazungu kutoka Uholanzi,Ufaransa na Ujerumani.Makaburu hao walihama kwenda kaskazini wakaanzisha jamhuri ndogo kati ya maeneo ya Waafrika ama kwa njia ya mapatano au kwa njia ya vita. Katikati ya miaka 1840 na 1850 Waingereza waliwafuata Makaburu kwa kuongeza maeneo yao hadi mto Oranje, waliteka jamhuri ya Kikaburu ya Natalia na kuanzisha koloni jipya la Natal. Jamhuri mbili za Makaburu ziliweza kustawi kwa miaka kadhaa ambazo zilikuwa jamhuri ya Dola Huru la Oranje upande wa kaskazini wa mto Oranje na jamhuri ya Transvaal (ilijiita pia Jamhuri ya Kiafrika ya Kusini) upande wa kaskazini wa mto Vaal.

Kutokana na kutanuka kwa kila miliki, Milki za Kiafrika zilitafuta njia zao kati ya himaya hizi za Wazungu ambao walikuwa na nguvu kutokana na silaha za kisasa.Wengine walitafuta uhusiano mzuri na Makaburu na kushikamana nao,wengine waliona Makaburu kama hatari wakatafuta uhusiano wa ulinzi na Waingereza. Mikataba kati ya Waingereza na milki za Kiafrika iliunda nchi lindwa zinazoendelea kama nchi huru kama vile Botswana (Bechuanaland),Lesotho (Basutoland) na Uswazi (Swaziland).

Katika miaka ya 1880 almasi na dhahabu zilipatikana kwa wingi katika jamhuri hizi na kusababisha kufika kwa wachimbaji wa. madini wengi, hasa Waingereza, waliotaka kutajirika; Makaburu walisita kuwapa haki za kiraia kwa sababu waliogopa wageni wengi. Tatizo hilo lilisababisha vita vya Makaburu dhidi ya Uingereza na jamhuri za Makaburu zilitwaliwa na jeshi la Kiingereza hadi mwaka 1902 zikawa makoloni ya Uingereza.

Jitihada za kupatanisha Wazungu wa Afrika Kusini (yaani Waingereza na Makaburu) zilisababisha kuundwa kwa Muungano wa Afrika Kusini kama nchi ya kujitawala ndani ya Milki ya Uingereza.Waafrika kwa jumla hawakuwa na haki za kiraia katika nchi hiyo ispokuwa katika Jimbo la Rasi kama walikuwa na elimu na mapato ya kulipa kodi za kutosha.


Baada ya vita kuu ya pili ya dunia Chama cha National kilichofuata itikadi kali kilipata kura nyingi na kuchukua serikali ya Afrika Kusini katika uchaguzi wa kwanza uliyoipa mamlaka Afrika kusini kujiamulia mambo yake yenyewe kwa kupatiwa uhuru na Uingereza. Hapo serikali mpya ilianzisha mfumo wa ubaguzi wa rangi ulio julikana kwa jina la apartheid. Haki za wasio Wazungu zilipunguzwa zaidi.Maeneo ya Kiafrika yalitangazwa kuwa nchi za pekee chini ya usimamizi wa serikali ya Kizungu ya Afrika Kusini,kwa hiyo wananchi kutoka maeneo hayo hawakuwa tena na haki za kukata rufaa mbele ya mahakama,walipewa vibali vya muda tu kukaa kwenye miji.

Waafrika walipaswa kutembea muda wote na paspoti na vibali, ndoa na mapenzi kati ya watu wa rangi tofauti zilipigwa marufuku.Shule na makazi zilitenganishwa. Siasa hiyo ilisababisha Mfarakano mkubwa kati ya nchi nyingi za dunia na Afrika Kusini.Upinzani na kutofautiana na Uingereza na Jumuiya ya Madola ulisababisha kuondoka kwa Afrika Kusini katika jumuiya hiyo na kufanya kujitangaza kama Jamhuri ya Afrika Kusini.

Kufatia harakati za ukombozi zilizofanywa na vyama vya PAC na ANC hatimae mwaka 1990 Apartheid ilikwisha na serikali ya National Party chini ya De Kreck ilipaswa kuendesha uchaguzi huru kwa wananchi wote kupitia mkataba wa amani na demokrasia wa "Freedom Charter" na kukabidhi madaraka kwa serikali ya ANC chini ya Nelson Mandela, kupitia uchaguzi uliofanyika mwaka 1994.

Hivyo tunaitakia Afrika kusini uchaguzi Mkuu mwema na wenye amani.... "Nkhosi Sikelei"

[emoji117][emoji420]Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
[emoji2400]Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
[emoji2398] Copy rights of this article reserved
[emoji2400]written by Comred Mbwana Allyamtu

Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com



 

EFF CIC Julius Malema rally keynote speech
 
Sure nakwambia, hao kina Malema ni wahuni tu wenye misimamo ya kihuni. Wakishinda hao utarudi kwenu usukumani bila chupi au boxer!
Acha kudaganya Watanzania walioshindwa hata kuitisha mikutano ya kisiasa
 
Sure nakwambia, hao kina Malema ni wahuni tu wenye misimamo ya kihuni. Wakishinda hao utarudi kwenu usukumani bila chupi au boxer!
Hahahahaaa lusungo umenifanya nicheke sana asubuhi hii eti bila chupi au boxer kwa taarifa yako shemeji yako ni ANC mie nilianza kufatilia siasa za Malema kabla hata sijazamia na nilikuwa namfananisha misimamo yake na Kamanda Mawazo marehemu
 
Mwingine atakwambia Mbowe amedumu sana kama mwenyekiti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…