Sophia Simba hafai kuwa Waziri wa Utawala Bora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sophia Simba hafai kuwa Waziri wa Utawala Bora

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 12, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1124
  Nov 12, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,510
  Likes Received: 5,741
  Trophy Points: 280
  Sophia Simba hafai kuwa Waziri wa Utawala Bora  pdidy.swi


  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Mnyambi Simba, kwa mara nyingine tena amezua mjadala na kuamsha hisia za waliosinzia kuhusu utata wa utumishi wake ndani ya Serikali ya Awamu ya Nne chini ya mwamvuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
  Ni mara nyingine kwa sababu huko nyuma amewahi pia kutoa kauli zenye ukakasi akimshambulia mfanyabiashara na mmoja wa wafadhili wa chama tawala kilichomweka waziri huyo madarakani.
  Ni huyu huyu Sophia ambaye chama chake kimekanusha matamshi aliyotatoa mbele ya kadamnasi kuwashambulia wabunge wa kuchaguliwa walio mume na mke – John Malecela na Anne Kilango Malecela.
  Ni huyu Sophia mwenye dhamana ndani ya wizara nyeti ya Utawala Bora, yenye wajibu wa kusimamia mienendo ya watumishi wa umma, iliyo chini ya Ofisi ya Rais.
  Ni Sophia ndiye anayewajibika katika kusimamia na kutekeleza kiapo chake cha utii na kumshauri vema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika masuala mbalimbali yenye maslahi kwa taifa, bila migogoro yoyote.
  Ni huyu Sophia, ambaye ndani ya chama chake, amekabidhiwa dhamana ya uenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) - wanaokiamini, kukipenda na kukitumikia chama tawala, yaani CCM.
  Ni huyu Sophia aliyedaiwa kumwangushia kipigo, aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Janeth Kahama, wakati wa mchakato na kampeni za kumtafuta mwenyekiti wa wanawake hao kwa njia ya kura.
  Ni Sophia huyu huyu, aliyewahi kukaririwa na vyombo vya habari akiwatetea wafanyabiashara wakubwa wanaotuhumiwa kwa ufisadi na kuzua gumzo na kuharibu upepo wa nchi wakati huo.
  Sophia Simba, kwangu ni mwanamama anayekurupuka. Ni Waziri asiyejipa muda wa kutafakari na kueleza anachokifahamu. Wakati mwingine nahisi anatumika ama kwa nia ovu au kwa maslahi ya taifa ili kuharibu mwelekeo ama kuwasahaulisha walalahoi kero zinazowakabili.
  Ni Sophia, aliyejaribu kucheza ngoma tofauti ya vita dhidi ya ufisadi iliyoanzishwa na viongozi wa vyama vya upinzani kabla ya kupokelewa kwa shangwe wa wakuu wa chama chake, akiwemo rais aliyemteua kushika nafasi ya uwaziri.
  Ni Sophia aliyewashangaza wasomi na wasio wasomi, pale alipojiinua na kuishambulia familia ya wanasiasa, akiwemo mkongwe, Mzee Malecela.
  Ni huyu Waziri Sophia aliyewaacha vinywa wazi wachambuzi, wajuzi na wananchi wa kawaida pale alipowashambulia kwa tuhuma mbalimbali wanasiasa wenzake.
  Ni wapi alipokuwa Sophia kiasi cha kuzikalia tuhuma nzito za wanasiasa hao na kujinasibu kwamba ndani ya chama chao cha CCM hakuna msafi, wote ni mafisadi?
  Ni imani yangu kwamba Sophia anahitaji kubanwa ili aanike tuhuma zote anazozifahamu, pengine atalisaidia taifa na kulirejesha kwenye mstari ili walalahoi waone raha na faida ya kuzaliwa juu ya ardhi ya Tanzania.
  Pamoja na yote, nina ushauri kwa mkuu wake wa kazi. Kwanza amfukuze kwa sababu amejidhihirisha kwamba hafai kuwa kiongozi wa wanyonge kwa sababu ameshindwa kusimamia mienendo ya watumishi wa umma. Sophia aanze kufuatiliwa, ahojiwe na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Polisi na Usalama wa Taifa. Ni Imani yangu kwamba kuondolewa kwa waziri huyu katika nafasi aliyonayo, kutabadili fikira zangu kwamba analipwa fadhila za mema machache aliyoyatenda wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005
   
Loading...