Kweli wataushangaza dunia kwa kupata 10% ya kura zote,Padri ajiandae kurudi mizabahuni!
watu kama ninyi ndio watu hatari amabao kwa ufinyu wenu wa mtazamo mnazalisha fikra ovu na mbovu.
Nani kakwambia udini wa mtu una manufaa kwa taifa? nani kakwambia Dk Slaa akienda ikulu anakwenda kufanya kazi ya kanisa?
Wapo watu wangapi katika historia ya dunia hii wamefanya mabadiliko makubwa na ya kutiliwa mfano ilhali walikuwa na historia ya kuhusika na dini kabla?
Mbona Dk Lwakatare alivyopewa ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya CCM watu kama ninyi hamkusema ilhali alikuwa active leader wa kanisa lake?
Mbona Uongozi wa juu Tanzania bara na visiwani ni wa kiislamu lakini hakuna anayesema?
Nitakwambia ni kwanini. Sababu ya msingi ni kuwa hatuko interested na dini ya mtu, bali uwezo wa mtu huyo wa kutimiza matakwa ya Taifa kwa ujumla. Hata kama Sheikh Gorogosi angegombea leo na akawa na fikra na misimao thabiti ya maendeleo ya taifa hili tutampigia kura bila kujali yeye ni Sheikh! Tunajua akienda ikulu haendi kuhubiri uislamu. Hali kadhalika angekwenda Kadinali pengo ama hata Kakobe, hatutajali udini wala historia yake ya dini kwakuwa udini wake ni irrelevant to the issues on the table!
Tunaangalia uwezo wa mtu husika na dhamira ya chama chake!
Je akisema atakuwa mkali kwa watendaji wa serikali tukimtazama tunaona anadhamira ya kweli katika kutekeleza hayo?
Hilo ndilo jambo la msingi tutakalojiuliza tutakapokuwa tukitafakari kabla ya kupiga kura.
Kwa hiyo watu kama ninyi mnaohubiri dini za watu hampaswi hata kuishi, (sorry for being so harsh, but it is the fact). Imagine watu wa aina yako mnaweza kuleta dosari kubwa namna gani miachwa mzungumze na watanzania wengi wasiojua kupambanua mambo?
Tunasema hivi, tunawatazama wagombea na vyama vyote vinavyoshiriki ktk uchaguzi, tunawapima na kuwatathmini, na jibu tunalopata ni kuwa wapinzani wana nia na dhamira ya kweli kutuletea maendeleo na kutufikisha pale tunapotaka kufika.
CCM wanacheza michezo michafu, ni wala rushwa, wanaamini katika rushwa na kubwabwaja - ushahidi wa kura za maoni ulionekana wazi!
Ktika upinzani wenye bidii ni CHADEMA na CUF, hatutajali nani zaidi lakini tunahitaji mpinzani kuwa rais mwaka huu tupime!
Kenya walimpa mpinzani, tizama leo wana katiba mpya na siasa za nchi ile zimechangamka! Uingereza na Marekani hali kadhalika. Watu wanaoamini katika kuutumia unyonge wetu kwa manufaaa yao na familia zao na maswahiba zao hatuwataki na nikisema hivyo namaanisha CCM hatuitaki!
Kura zote safari hii kwa upinzani.
Kuna wale wanamkosoa mgombea mwenza wa CHADEMA kuwa ameishia darasa la saba, nawauliza: So what? Zuma wa Afrika kusini has never seen an inside of a formal class, kwa hiyo ukimfanyia tathmini utaona hakusoma, but he is talent, has charisma etc and he is in the driving seat of his country!
Tunataka sera wala sio bwabwaja za CCM. Tangu lini maendeleo yakahitaji kusimuliwa? Watu si wapo wanatakiwa kuyaona wenyewe? Nani anahitaji takwimu? Kumbe ndo maana mmeamua kufanya elimu yetu kuwa kichwa cha mwendawazimu ili tusielewe kuchambua na kupambanua mambo muendelee kututawala kwa rushwa na uongozi mbovu tena? Katu hatutakubali! TUMECHOKA, safari hii ni upinzani, kwa uchache wao tumeona matunda yao ktk bunge lililopita. Nawaasa wananchi, wabunge madiwani na raisi safari hii ni wapinzani. Na kwa mtazamo wangu ni DK Slaa anayefaa!
Toa mtizamo wako, fanya maamuzi yako! Alicho-accomplish Dk Slaa kwa resources alizokuwa nazo kama mbunge ni kingi kuliko alicho accomplish Kikwete na resources zote zilizokuwa ta his disposal kwa muda wa miaka mitano!
Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki watu wetu!