Slaa: CCM wanafiki



Kweli kabisa wala hajadanganya na kila mtanzania anajuwa hivyo.
 
Dr. Slaa aache usela muda umeshamtupa mkono atafute mke aoe.
 
ni wanafiki sana ccm kule mtwara sasa vimeletwa vifaru vinne nya nini? afu wakti huohuo kulikuwa uzinduzi wa kiwanda cha saruji cha dangote na kuanza kusema wenyewe kuwa wale wachochezi wapate aibu. wanasahau kuwa wao ndio waanzilishi wa fujo za mtwara. ccm ni kweli wanafiki.
 
Kumbe haya yote yametolewa kupitia Tanzania daima, basi hapa hakuna habari kuna UDAKU!
 
kilichosahahulika hapo ni unafiki kwa kauli zinazotolewa sasa hivi na ccm kuhusu Gesi ya Mtwara
 
Tanzania Daima ni gazeti pendwa la udaku kama Uwazi na Kiu.
 
Dr. Slaa ndiye mnafiki kwasababu anatuambia anaweza kuliongoza taifa letu lenye watu zaidi ya milioni arobaini wakati ameshindwa kuiongoza familia yake isiyozidi watu kumi.

Kama suala la familia lina uhusiano na uongozi mbona Kikwete nchi ina mshinda japo kuna habari ana wake wa tatu? na kuna habari pia kwamba kamuoa mtoto wa Meighj hivi karibuni kwa siri lakini hii haijamuongezea ufanisi katika kuongoza Nchi yetu
 
Well said dr the gambaz ni wanafiki kabisa wa kwanza ni sitta.

Huyo mheshimiwa angemaliza sakata la Richmond vizuri kama alivyolianza ningempa kura yangu ya uraisi. Kilichotendeka pale ni "mwenzetu au wenzetu" na hii ndio inaimaliza CCM kweupeee!
 
Dr.slaa wewe ni mkweli siku zote hilo halina ubishi na mungu akulinde na akupe maisha marefu uendelee kuwakosoa hawa chekechea wa ccm.

Dr. Ninaombi moja kwako,
Nina wasiwasi kuna mchezo chafu utachezwa kwenye chaguzi za kata na wapinzani wako ccm ili wapate pa kutokea baada ya lwakataregate kufail.Na huenda kweli msishinde hata kata moja kama hamtakaa na kubaini ni mpango gani ccm wamepanga.Kwa kuwasaidia nendeni ktk vitongoji vya singida mlikoshindwa mkajifunze kwani mbinu iliyotumika ndiyo hiyohiyo itatumika kwa uchaguzi wa madiwani 25.CCM wamejipanga kuwaduwaza ndiyo maana hawahangaiki na majukwaa wana lao la kuwatoa .chunguza mjomba utabaini
 
Kuna unafiki mbaya kama kutelekeza familia yako halafu unajifanya kusomesha yatima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…