Tuwe wakweli huyu sasa ni unafiki wa hali ya juu!!
CDM haikumtambua rais Kikwete kwamba hakuchaguliwa kihalali 2010 na wakatoka nje ya bunge, lakini baada ya muda kwa maslahi ya taifa wakamtambua na viongozi mbalimbali wa CDM wamemwalika kikwete katika hafla zao na kumpongeza kwa mafanikio flani, alianza Dr Slaa alipomwalika JK kwenye hafla ya uchangiaji wa CCBRT, Kikwete alipokuwa Kilimanjaro wabunge wale walishiriki kwenye ziara zake na wakampongeza kwa mafanikio yake, mbona hawakukemewa na yeyote hawa? kwa kuwa ni viongozi wakubwa?
Madiwani hawa wadogo wameshiriki kwenye suala la jiji wanaambiwa Meya hakuchaguliwa kihalali, hivi kwa nini isifike wakati CDM ikubali kwamba tugange yajayo kwa manufaa ya wananchi? leo maamuzi na hoja za madiwani wa CDM hazifanyiwi kazi ila wanaoathirika ni wananchi, je, CDM inakosa huruma na hawa wananchi?
kuna ishu ya posho, madiwani wanalaumiwa kwa kuchukua posho, lakini bungeni CDM msimamo wake rasmi ni kutochukua posho hizo, wabunge kadhaa kama Shibuda, Selasini na Msigwa walisema wao hawataziacha na wabunge wengine kisirisiri hawaziachi isipokuwa Zitto, mbona hatumsikii Slaa akiwakoromea hawa kwamba wameenda kinyume na msimamo wa chama? je adhabu hizi si kwamba ni kwa wadogo tu?
muhimu, chama kfanye maamuzi ambayo hayawaathiri wananchi, wanachama wapewe adhabu ndani ya chama lakini maamuzi hayo yasiwaumize wananchi, vinginevyo wanachi wanaweza kujuta kwanini waliichagua CDM na next election wakaamua otherwise