Mimi nadhani Sitta hana cha kujadili kwenye huo mdahalo kwa kuwa yote ameshayamaliza. Kasema kuwa total package ya mbunge ni 7m. Dr Slaa alisema hivyo hivyo, total package ni 7M. Kama allowance za jimbo anapewa mbunge kwenye pay check yake ya mwezi, ina maana it is his money!! anaweza kuzitumia apendavyo. Kwa nini kila jimbo lisiwe na ofisi ya mbunge, ambayo hiyo allowance itapitishiwa huko kiofisi, kwa nini anapewa mbunge kama package yake-- kimsingi huo ndio mshahara wa mbunge!! Huo mchanganuo wa Sitta ni semantics tu na hauna credibility ya kuomba mdahalo
Kuhusu suala la elimu, anasema kuwa lazima kuwepo na mipango, na maandalizi etc. Sidhani kama Slaa anataka kuanza na watoto wapya kabisa wa kusoma bure, what is needed ni kusema tu kuwa kuanzia sasa hakuna mwanafunzi wa shule ya serekali kudaiwa ada, au kupeleka dawati, simple, hilo linahitaji mpango gani na maandalizi gani, since vyanzo vingine vya fedha vya kuziba hilo pengo vimeanishwa kwenye ilani ya chadema-- Mr Six asome tu ilani ya Chadema na majibu yako wazi, besides, huwezi kudetail hizo specifcs kwenye mkutano wa hadhara, nani atakuelewa, hata JK anavyoahidi hatoe specifics jamani, anatoa blanket promises tu
Dr Slaa, ukipenda unaweza kufanya mdahalo na Six huko huko Urambo utakapofika huko, Six aje tu kwenye mkutano wako na akuulize maswali yake yanayomsumbua, si lazima aje Dar, afterall Dr Slaa hayuko DAR na mdahalo si lazima ufanyike Dar-- huyu six naye kwa kukariri, lol,.