Sitta amdharau kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta amdharau kikwete

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Plato, Sep 16, 2010.

 1. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  Baada ya masha kumdhalilisha kikwete kuhusu uraia wa bashe, spika sita naye ameongeza zaidi.amedai kuwa dr.slaa ni saizi yake,wawe na mdahalo na wamuache kikwete afanye kampeni tu.
  Tunajua kikwete kaogopa mdahalo na slaa.sasa sitta anasema yeye ndiye saizi ya slaa.yarabi toba! Wakimnyima uspika huyu,na kumnyang'hanya kadi, mimi simo,au kama ilivyokuwa kwa bashe wakisema si raia msinifuate
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  huo ndo ukweli mara mia ya sitta kuliko JK , kwa hiyo kama ni mdahalo wafanye slaa na sitta sio mkwere.
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mimi naona sitta kamdharau zaidi slaa kwamba hana ubavu na mdahalo with CCM presidential candidate labda apewe mgombea ubunge ndio saizi yake

  its all perception
   
 4. hope 2

  hope 2 Senior Member

  #4
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 155
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ni kweli Mkuu, tunataka wenye kugombea kiti cha urahisi wafanye mdahalo wao kwa wao,
  Hizo ni dharau
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,577
  Likes Received: 18,524
  Trophy Points: 280
  Sitta hajamdharau JK bali anajiamini kuhimili midahalo, he has confidence ambayo JK lack!.

  Enzi za kipindi cha Kiti Moto, CCM walikuwa wanakigwaya hicho kipindi na kuna mpuuzi mmoja kigogo wa CCM alihakikisha kinafungwa. Mwendeshaji wake, aliwahi kukutana na Lawassa mahali, Lowassa akamwambia yeye alikipenda kile kipindi, ni bahati mbaya kimekufa!.

  Hivyo hili zuio kwa wagombea wa CCM kutoshiriki midahalo ya TBC ni la kienda wazimu tuu, linalotokana na kutojiamini kwa baadhi ya vilaza wa CCM kuogopwa kugalagazwa!.

  Naamini wako baadhi ya wagombea wa CCM ni majasiri na ni watu wanaojiamini, sio tuu hawaogopi midahalo, bali wangependa kushiriki na wangefunika mbaya, ila huo uendewazimu wa baadhi ya viongozi wao, wamewazima midomo.

  Sorry Mode, kama itaonekana nimetumia lugha kali sana, naomba nitairekebisha, sio madhumuni yangu, bali nimekasirika sana na uamuzi huu wa kiendawazimu wa CCM kutoshiriki midahalo!.
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ni kweli kabisa pasco

  sitta is confident, but to me nadhani itakua insult kwa slaa kufanya mdahalo na mgombea ubunge... its degrading
   
 7. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Sitta apambanishwe na Tindu Lisu
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwani Urambo Mashariki ni Nchi? Sitta afanye mdahalo na Zitto.
   
 9. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sitta kamtukana Kikwete hiyo haina shaka! Ameonyesha yeyew kuwa ni jasiri kuliko kikwete, ameonyesha kuwa kikwete hawezi kummudu Dk slaa, ameonyesha kuwa kikwete hakufaa kugombea urais kwa sababu ameisha onekana kuwa hana ubavu wa kulinganishwa na Dk wa kikweli, amemdhalilisha kikwete kwa ku dare na kutaka kufanya kitu ambacho kikwete anaona hakiwezekaniki . Sitta ana matusi ya rejareja maana si mara ya kwanza kufanya hivyo!

  Aliisha wahi kumtukana kikwete akimwambia kuwa yeye na marafiki zake wanaendesha siasa za majitaka
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  A thing that can not live to see a day!

  Sitta yuko entitled kusema chochote, lakini kwa hakika anajua kabisa materially ni kwa jinsi gani Slaa alivyo kichwa!
  Kauli zingine za wanasiasa ni za kuzipuuza tu!
   
 11. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Dr. Slaa ni mgombea Urais, hatakiwi kufanya mdahalo na mgombea Ubunge, labda kama mdahalo utahusu mambo ya Urambo
   
 12. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huko ndiko kumdharau kwenyewe mzee!
  Amemtukana kwamba hana confidence na hana uwezo wa kusimama mbele kushindana na Dk Slaa
   
 13. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivi huyu hajasikia agizo la Makamba? Au amewasahau CCM walivyotaka kumchakachua!!!!!!!
   
 14. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Sitta ajitwika zigo la CCM Send to a friend Thursday, 16 September 2010 07:41 0diggsdigg

  [​IMG] Samweli Sitta

  Waandishi Wetu
  MAKOMBORA ya Dk Willibrod Slaa dhidi ya spika anayemaliza muda wake, Samuel Sitta, yamezidi kuongeza joto la kampeni za uchaguzi baada ya kada huyo wa CCM kutangaza kuwa anataka mdahalo wa wazi na mgombea urais huyo wa Chadema ili kuondoa kile alichokiita siasa za ulaghai na upotoshaji.Vyama vya Chadema na CUF vimekuwa vikitaka mdahalo wa pamoja na mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete lakini chama hicho tawala kimesema kuwa mgombea wake hana haja ya kitu kama hicho na kikaenda mbali zaidi kwa kutoa waraka wa kupiga marufuku wagombea wake wa ubunge na udiwani kushiriki kwenye midahalo hadi kwa maelekezo maalum.

  Lakini jana, Sitta aliiambia Mwananchi kuwa yuko tayari kushiriki mdahalo na Dk Slaa baada ya katibu huyo mkuu wa Chadema kumshambulia kuwa ni mnafiki kutokana na kupinga sera ya chama hicho cha upinzani ya kutoa elimu bure kwa wote.

  Dk Slaa alimshambulia Sitta juzi akiwa mkoani Mara ambako alisema katika uongozi wake wa uspika alizima kashfa nzito za ufisadi, likiwemo sakata lililotikisa nchi la zabuni ya ufuaji wa umememwa dharu iliyokwenda mikononi mwa kampni ya Richmond Development LLC, wizi wa fedha kwenye akaunti ya EPA, ufisadi wa kampuni za Deep Green Finance na Meremeta.
  Dk Slaa, ambaye alipata umaarufu kutokana na kuibua kashfa mbalimbali, alimuelezea mbunge huyo wa Urambo Mashariki kuwa alimzima wakati alipokuwa akipinga mishahara mikubwa ya wabunge na kumwita kuwa ni mnafiki.

  Jana, akizungumza na Mwananchi kutoka jimboni kwake, Sitta alisema: "Kwanza namuonea huruma sana Dk Slaa; siasa zake za ghilba zinaonyesha ni mtu aliyekata tamaa kwamba atashindwa na hafai kuwa rais. Anafanya siasa za ulaghai.

  "Yeye ndiyo mnafiki mkubwa na mlaghai. Anasema mbunge anapata mshahara Sh7 milioni, lakini katika miaka 15 ya ubunge hajawahi kusamehe mshahara hata mwezi mmoja. Kusema bila vitendo ni unafiki, hilo analosema lingekuwa dhamira ya kusaidia umma, basi angekataa kuchukua mishahara miezi yote."

  Kwa mujibu wa Sitta, ambaye alisifika kwa kuruhusu mijadala mizito dhidi ya serikali, kauli anazotoa Dk Slaa kuomba kura kwa wananchi zinamkera kwa sababu zimejaa upotoshaji na ulaghai na kuongeza kusema: "Natamani ningefanya mdahalo naye leo hii."

  "Ningekuwa Dar ningeomba kufanya mdahalo na Dk Slaa ili aeleze hayo anayosema nami nifafanue. Bahati mbaya nipo kilomita takriban 1,000 kutoka Dar. Lakini, ili kuondoa ulaghai wake kwa wananchi nataka mdahalo na Dk Slaa; mimi ndiyo saizi yake si Kikwete. Kikwete amwache apige kampeni tu," alitamba Sitta.

  Kuhusu hoja ya mishahara mikubw aya wabunge, Sitta alidai Dk Slaa anapotosha umma anaposema mbunge anapata mshahara wa Sh7 milioni. Alisema kuwa mbunge anapata mshahara kamili wa Sh2 milioni, akiwa katika daraja la saba la mshahara wa viongozi (LSS).
  Hata hivyo, alisema hesabu za Dk Slaa zinajumuisha fedha nyingine ambazo ziko nje ya mshahara, ikiwa ni pamoja na fedha za mafuta, kuendesha ofisi ya mbunge ambazo ni za jimbo.

  "Dk Slaa aonyeshe hati ya malipo ya mshahara unaoonyesha mbunge analipwa mshahara halisi wa sh 7 milioni," alisema Sitta.
  Sitta, ambaye amemaliza kipindi cha kwanza cha miaka mitano ya kuongoza chombo hicho cha kutunga sheria, alisema: "Kujumuisha fedha za kuendesha ofisi na mshahara ni sawa pia na kujumuisha fedha za kuendesha ofisi ya katibu mkuu wa wizara katika mshahara, huu ni ulaghai tu... wala hii haingii akilini."

  Alisema mbunge anapata mshahara mdogo kuliko hata mkuu wa wilaya ambaye yuko daraja la LSS6 na "sijui kama anafanya utafiti, lakini alipaswa kuzikataa fedha za mshahara; mbona alikuwa anapokea? Alianza kujenga hoja hii baada ya kuona anataka kugombea urais, Slaa aache ghilba".

  "Ndiyo maana, nasema nina wasiwasi Dk Slaa anatoa ahadi ambazo hakuzifanyia utafiti. Unajua huwezi kuwaambia watu tu kwamba utatoa elimu bure ya hadi kidato cha sita. Hebu waeleze wanatarajia kuanza na wanafunzi wangapi, wamekokotoa hesabu watatumia shilingi ngapi kwa kuanzia na malengo hayo ni kwa muda gani na mtoto mmoja gharama yake ni shilingi ngapi," alieleza.

  "Kwabababu kufanya siasa za ulaghai kwa wananchi ili upate madaraka ni kosa baadaye itakuja kuleta matatizo. Sina tatizo na watu kusomeshwa bure, lakini tunataka ahadi zilizofanyiwa utafiti ambazo zitamkomboa mwananchi kweli."

  Dk Slaa kuipiga bei ndege ya Rais
  Naye Dk Slaa, ambaye anaendeleza na ziara zake za kampeni, jana aliendelea na sera zake za kupunguza matumizi ya serikali alipoeleza kuwa ataiuza ndege ya rais ambayo alidai kuwa Kikwete amekuwa akizurura nayo nje ya nchi kufanya anasa kwa kodi za wananchi.
  Akihutubia wananchi wa Sirari mkoani Mara, Dk Slaa alisema ndege hiyo imekuwa ikitumia kiasi cha Sh6 milioni inaporuka kwa saa moja kitu ambacho ni cha kifisadi
  .
  Dk Slaa alisema kuwa Kikwete amekuwa akifanya safari za kupindukia nje ya nchi tangu aingie madarakani mwaka 2005 na kulitia taifa hasara, kitu ambacho alisema ni hatari.
  "Anadai kuwa anatafuta wawekezaji lakini cha kushangaza nchi inazidi kushuka kwa ubora kiuwekezaji... sasa imekuwa nchi ya 131 kutoka 121," alisema Dk Slaa.

  Dk Slaa alisema kutokana na ndege hiyo kutumia fedha nyingi ambazo hazina tija kwa Watanzania, akiingia ikulu ataiuza na kununua helkopta ambayo inaweza kutua kila kijiji na kutoa huduma kwa wananchi tatizo linapotokea.
  "Helkopta haitumii gharama kubwa kama ilivyo ndege hiyo, hivyo ni bora kuiuza kwa kuwa ni ya kianasa zaidi," alisema.

  Alisema Kikwete hufuatana na msafara mkubwa wa watu ambao wamekuwa wakilipwa fedha nyingi na kulala hoteli za gharama kubwa zisizokuwa na msingi katika maendeleo ya taifa ambalo wananchi wake ni masikini.

  "Katika safari yake ya mwisho kwenda Marekani ambayo alipitia Dubai, mmoja wa maofisa wake alinunua magari mawili baada ya kurejea nchini kutokana na posho za safari hiyo.

  Hii ni hatari na haifai kabisa na mbaya zaidi amekuwa akifikia na msafara wake wote katika hoteli za gharama ya dola 5,000 za Kimarekani kiwango ambacho ni cha anasa," alidai Dk Slaa.

  Akiwa Kata ya Nyamongo ambako uko mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya Barrick, Dk Slaa alisema kuwa atafumua mikataba ya migodi hiyo mara atakapoingia madarakani kwa kuwa wananchi wanaishi karibu na migodi hiyo hawafaidiki na maisha yao ni duni.

  "Rasilimali za taifa hili ni lazima tuzirudishe kwa wananchi ili tuweze kuboresha maisha yao, hivyo nitahakikisha migodi hii na mikataba yake inafumuliwa ili tufaidike wote,"alisema Dk Slaa.

  Alisema kuwa hata polisi ambao wamekuwa wakiwapiga wananchi wanaokaa karibu na mgodi wa North Mara hawataweza kufanya hivyo tena kwa kuwa mgodi huo utakuwa mali ya wananchi wa Nyamongo na Tanzania kwa ujumla.

  Dk Slaa pia alimtaka Kikwete aache kuwa mnafiki kama Sitta kutokana na kueleza kuwa elimu ya bure haiwezekani wakati wanajua ukweli kuwa inawezekana.
  Alisema kuwa wanaujua ukweli kwa kuwa enzi za mwalimu walisoma bure na ndiyo maana leo wanaringa kwa kuwa walisoma bila tatizo lolote.

  "Simuelewi Kikwete kwa kuwa haeleweki na hajui anachosema... ni mtu wa kuona noma (haya) kusema ukweli mbele ya wananchi, hivyo aache kuwadanganya kwa kuwa hivi sasa hawadanganyiki," alisema Dk Slaa.

  Dk Slaa alisema kuwa Kikwete anakumbuka wakati alipokuwa waziri alipitisha sheria ya kusamehe kodi kwa miaka mitano kwa wawekezaji, kodi ingeweza kutumika kuwasomesha wananchi bure.

  "Kikwete yuko tayari kumwezesha mzungu na si Mtanzania masikini anayeishi maisha duni," alisema.

  Dk Slaa pia alisema risiti ya malipo ya kumkodishia ndege ya serikali Mama Salma Kikwete zilizoonyeshwa na meneja wa kampeni za CCM, Abdulrahaman Kinana zina shaka na inabidi zichunguzwe.

  "Waichapishe kwenye magazeti yote ili wananchi waione lakini pamoja na hayo nikiingia ikulu nitaichunguza," alisema Dk Slaa.

  ...CCM wajibu mapigo

  Katika hatua nyingine, CCM imejibu tuhuma zilizotolewa dhidi ya Mama Kikwete anayedaiwa kufanya matumizi mabaya ya fedha za serikali ikiwemo ndege za serikali katika kampeni zake, ikisema kuwa ndege hizo hukodishwa kwa Wakala wa Ndege za Serikali.

  Mratibu kampeni wa CCM, Abdularhaman Kinana aliwaambia waandishi jijini Dar es Salaam ndege hiyo hukodishwa na chama hicho.

  "Ndege za Wakala wa Ndege za Serikali zinakodishwa kwa mtu yoyote ili mradi ratiba zisiingiliane na za viongozi. Mara nyingi watu huzikodi kwa ajili ya kufanikisha mazishi... ni ruksa kukodi ndege hizo ili mradi umudu kulipa gharama zake," alisema.
  Alisema taasisi hiyo inajiendesha kibiashara kwa kujitegemea.

  "Ukiiona ndege ya serikali inasafiri ufahamu kuwa imekodishwa, hata gharama zake ziko wazi, kila mahali unaposafiri ukifika ofisini kwao watakueleza gharama zao," alisema.
  Kinana aliwaonyesha waandishi wa habari risiti ya kukodi ndege ya serikali 5HT GF iliyompeleka Mama Kikwete Musoma akitokea Dar es salaam. Inaonyesha kuwa gharama za kukodi ndege kwa safari hiyo ni Sh.22 milioni.

  Alisema mbali na ndege za serikali, huwa pia wanakodi ndege binafsi kwa ajili kumsafirisha mke wa rais kwenda katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya kampeni.
  Alisema Mama Kikwete ataendelea kufanya kampeni kwa kwa gharama zozote za chama hicho kwa vile kimeona kuna tija kwa yeye kampeni.

  Kinana alisema Dk Slaa anaonekana kuishiwa hoja kwa kuwa alitakiwa kufanya utafiti kwanza kabla ya kutoa tuhuma ambazo hazina ukweli wowote.

  "Tunasikitika kuona kila siku Dk Slaa anafikiria namna ya kufungua kesi na kutoa tuhuma badala ya kuelekeza nguvu zake katika kunadi ilani ya chama chake. Hii inaonyesha jinsi mgombea huyo alivyoishiwa kisiasa," alisema.

  CCM yaivimbia Nec

  CCM pia imesema kamwe haiwezi kuondoa mabango yake sehemu mbalimbali nchini kama inavyoelekezwa na Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) kwa vile ujumbe uliopo kwenye mabango hayo unaonyesha namna chama hicho kilivyotekeleza ilani yake.

  Alisema wameiheshimu Nec kwa kuondoa mabango mawili yanayomwonyesha Rais Kikwete akiwa na majaji na nyingine lenye picha ya mgombea huyo akikagua jeshi.

  "Tunasema tumeondoa mabango hayo, lakini hatuwezi kuondoa mabango mengine kwa vile hatuoni sababu kwa kuwa rais anaonyesha namna alivyotekeleza ilani ya chama chake," alisema.
  "Mbona kuna mabango ya wagombea urais wa Chadema na CUF ambayo yanawaonyesha kuwa ni marais badala ya kusema wagombea urais, ina maana Nec haiyaoni," alihoji Kinana.

  Source: Mwananchi


  Taarifa hii imeandikwa Ramadhan Semtawa, Boniface Meena na Raymond Kaminyoge.
   
 15. minda

  minda JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  ni wazi mpaka sasa ameshanyimwa kwani kuwadi wake, malecela aka tingatinga, keshadondoshwa na kibajaj na swahiba zake; mpendazoe na shibuda wameshaona ukweli na kuchukua hatua mwafaka.
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Sitta ni mmoja wa watu wanaoweweseka na CCM inavyokwenda... Credit to Kikwete for keeping most political allies guessing though
   
 17. n

  nmaduhu Member

  #17
  Sep 16, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii ni dharau kwa Jk, yaani ccm wamekosa kabisa dira, hivi uamzi wa ccm kukataa mdaharo nani aliutoa?? kwa ninavyojua ule ni uamzi wa
  uongozi wa juu wa chama, na Sita najua ni mwanakamati kuu, sasa iweje leo anatokea na kuanza kupingana na uamzi wa uongozi wa juu
  wa chama chake, hapa ndo mtaelewa ni kwa nini Masha naye akaamua kutofautiana na Jk.......
   
 18. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2010
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,561
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Damn right kaka.
   
 19. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  [font=&quot]samwel sitta hana lolote bali analamba matapishi yake mwenyewe, kama angekuwa jasiri na mtu asiyejali maslahi binafsi angewakoromea mafisadi katika vikao vya cc na nec ya ccm walipotaka kumnyang'anya kadi na kumvua uspikia.
  [/font]

  [font=&quot][/font]
  [font=&quot]mwanasheria mzima alinywea na hakufurukuta na kukubali kudhalilishwa na "malumpen" waliojaa katika vikao kama kina g*****ta na wengine. [/font]
  [font=&quot]hapo tukagundua kuwa mhe sitta hana ujasiri wa kusimamia misingi ya baba wa taifa ila ni mganga njaa kama weznie waliokuwa wakimsulubu kwa kuwasaliti.[/font]

  [font=&quot][/font]
  [font=&quot]alishindwa kuuthibitisha umma wa tanzania kuwa ccm sio baba na mama samwel sitta.
  [/font]

  [font=&quot][/font]
  [font=&quot]kama s sitta anautamani mdahalo wa wagom,bea urais mbona hakujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo wakati ccm ilipotangaza kutoa fomu kwa ajili ya nafasi hiyo? Alimgwaya sheikh yahya?
  [/font]

  [font=&quot][/font]
  [font=&quot]katika mdahalo anataka kutetea kitu gani? Watuhumiwa mbali mbali wa ufisadi wakiwemo rostam, lowassa, chenge, karamagi, mramba na wengine wengi kupitishwa na ccm kugombea ubunge na nafasi mbali mbali za uongozi katika ccm na serikali ya tanzania?

  Hii ndio misingi ya baba wa taifa mwalimu nyerere samwel sitta aliyodai kuisimamia?

  Kabla ya kutaka mdahalo na dr slaa tunaomba awaelezee watanzania matumizi mabaya ya magari ya bunge ikiwemo toyota land cruiser (shangingi) 8 cylinder namba ya usajili stk 3002 na magari mengine mawili ambayo katika uspika wake yaliwekwa maalum kumhudumia yaye na nyumba zake ndogo. Achilia mbali magari ya serikali yanyotumika kuihudumia familia ya sitta kutoka wizara mbali mbali alizopitia mke wako

  mafisadi wakubwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  [/font]
  [font=&quot]watoto wa mwalimu nyerere walisoma shule za kawaida na watoto wa wakulima na wafanyakazi, iweje watoto wa nyumkba ndogo ya samwela sitta wapelekewe maua ya graduataion kwa kutumia gari za serikali kama sio ufisadi

  [/font]
  [font=&quot]heshima imeshuka


  [/font]
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Sep 16, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,577
  Likes Received: 18,524
  Trophy Points: 280
  MWANALUGALI, sio lazima awe amentharau JK, labda anamaani JK ni juu sana kwa Dr.Slaa, hivyo saizi yake ni yeye Six.
   
Loading...