Practically team inayofunga magoli kipindi cha 2 huwa inaogopwa zaidi kwakuwa inadhihirisha ubora wa benchi lake la ufundi katika kusoma madhaifu ya team pinzani na kuyafanyia kazi kwa kushusha maangamizi kipindi cha 2,ni style inayotumiwa na team zote zenye mafundi wazuri kwenye ma'benchi yao,angalia matokeo mengi ya Borusia na Bayern utakubalina na mimi katika hilo.Fikiria sasa takuwaje siku ya kufunga pazia la Ligi kuu ya msimu huu team mahiri katika KUTUPIA kipindi cha 2 (Yanga) itakapokutana na team maarufu kwa KUTUPIWA kipindi cha 2 (Simba) rejea matokeo yake dhidi ya team za Kagera,Toto na Azam.
Binafsi sina wasiwasi kabisa na mechi salia,pamoja na kuwa siku ya Mei Mosi Yanga itacheza dhidi ya team 3 za Coastal,Simba na Azam) lkn hiyo haitaizuia kudhihirisha uma kuwa msimu huu walijiandaa na Uturuki walikwenda kufanya kazi ya kujifunza na si kazi ya kufungasha kama hawa:-
Mmoja wa wachezaji wa Simba alipokuwa akirejea kutoka Oman walipoweka Kambi kuhakikisha wanajiandaa vizuri katika kuutetea u'bingwa wao ambao hata hivyo wameshavuliwa kitambo.
Kiungo mahiri wa Simba akirejea na matunda ya Kambi ya Oman yaliyoambatana na tambo kibao za kushusha maangamizi kwa team pinzani katika duru la 2 hata hivyo Vijana hao wa Malkia wa Nyuki walijikuta wakishushiwa maangamizi zaidi kuliko wao kushusha.