Siri ya Yanga yafichuka!

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
SIMBA na Coastal Union ambazo zimeshikilia ubingwa wa Yanga zimepata siri nzito ya Yanga ambayohuenda wakaitumia kuwadhibiti kwenye mechi mbili zilizosalia ambazo ni muhimu kwa heshima ya Yanga.
Sare yoyote dhidi ya Coastal Union Mei Mosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam itatosha kuipeleka Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2013/14ambao uongozi umepanga kusajili wachezaji wapya watano tu.
Lakini Yanga ambao ndio gumzo kwa sasa kwenye Ligi Kuu Bara siri yao imefichuka baada ya kubainika kwamba wamekuwa wabaya zaidi kwenye kupachika mabao dakika 45za pili kuliko za kwanza.
Tathmini inaonyesha kwamba timu hiyo imeshinda mechi sita kwenye dakika 45 za mwisho na nyingine tano zilizosalia ambazo ni chache imeshinda kipindi cha kwanza jambo ambalo limewapa kiburi maadui wake na linaweza kuiponza katika harakati zake za kusaka pointi moja ya ubingwa kwenye mechi mbili zilizobaki.
Yanga ina pointi 56, tisa mbele ya Azam yenye pointi 47 na Kagera Sugar ni ya tatu ikiwa na pointi 40 wakati bingwa msimu uliopita, Simba wakiwa nafasi ya nne na pointi 36.
Ingawa benchi la ufundi la Yanga limedai timu yao kukamiwa na timu ndogo ambazo zinang'ang'ana katika janga la kushuka daraja na pia kuzorota kwa safu ya ushambuliaji ya timu hiyo imechangia jambo hilo na kusababisha kutopata ushindi katika dakika za mwanzo na kusubiri hadi kipindi cha pili.
Yanga imevuna pointi 14 katika michezo sita baada ya kuifunga Ruvu Shooting bao 1-0 dakika ya 48, ikaibamiza Kagera Sugar bao 1- 0 dakika ya 70, ikaichapa Toto African bao 1 - 0 dakika ya 78, ikaifunga Prisons mabao 3-1 moja likifungwa kipindi cha kwanza mawili ya ushindi yakifungwa dakika ya 56 na 65.
Pia walitoka sare ya bao 1 - 1 na Mtibwa Sugar huku Yanga wakisawazisha bao hilo dakika ya 85 baada ya Mtibwa kutangulia kufunga walifanya hivyo pia katika mechi dhidi ya Mgambo iliyoisha kwa sare ya bao 1- 1 na Yanga kuchomoa bao hilo dakika ya 85 baada ya kutanguliwa kufungwa.
Mechi ambazo Yanga imefunga mabao katika kipindi cha kwanza ni dhidi ya Azam walioshinda bao 1 0 dakika ya 32, dhidi ya Oljoro waliyoshinda mabao 3 - 0 yote wakifunga kipindi cha kwanza, dhidiya African Lyon waliposhinda mabao4 - 0, mawili yakifungwa kipindi cha kwanza na mawili cha pili, dhidi ya JKT Ruvu waliposhinda mabao 3 - 0, moja likifungwa kipindi cha kwanza na mawili kipindi cha pili wakati walitoka suluhu mechi moja na Polisi Morogoro.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Fred Felix Minziro alisema: "Kuna timu zinang'ang'ana kutoshuka daraja hivyo ukikutana na timu hizo mechi huwa ngumu zaidi maana wanakukamia, sasa usipokuwa mjanja unaweza usiambulie kitu lakini hata hivyo nashukuru wachezaji wangu wamepambana na kupata ushindi, hata kama magoli yalikuwa yanapatikana kipindi cha pili lakini muhimu pointi tatu."
"Ingawa washambuliaji nao wanatakiwa kulaumiwa, kwani kaziyao ni kufunga mabao lakini kwenye timu yetu jambo hili ni tatizo kubwa, tumekuwa tukipata nafasi nyingi lakini magoli hayapatikani," alisema Minziro.

CHANZO: M/SPORTS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…