duniani kuna mambo mengi, unaweza ukajiuliza kwanini manufacture wakubwa kama NOKIA au BLACKBERRY wanatengeneza simu bila camera? na usipate majibu. ila jibu ni rahisi tu simu zisizo na camera ndio pekee huruhusiwa kwenye maeneo nyeti kwahio wafanyakazi wa maeneo nyeti wanatakiwa wawe na simu zisizo na camera. hapa nitaelezea simu nzuri zisizo na camera kwa ajili yao. nitazigawanya kwa kutumia operating sytem.
ANDROID; INO dualsim 3g ino sio manufacture anayefahamika sana ila amejitahidi kuwajali watu wasiotakiwa kuwa na simu zenye camera kwa kuwapa android. simu hii ina 2gb internal na memory card hadi 32gb (inakuja na 8gb pre loaded) processor 1ghz na ram 512mb. ina kioo cha inch 4 na resolution ya 480x800. bei ya hii simu ni around 400,000 kwa hela za tanzania.
JAVA PHONE: nokia 207 hii si smartphone ni feature phone ila yenye uwezo wa internet na 3g simu hii haina camera imetoka juz juz inauzwa dola 62 na nokia possible tz ikawa 120,000.
hizi ndo simu latest zisizo na camera ila pia zipo za zamani kama nokia e50, e51 za symbian na blackberry 8820, 8830 (hazina 3g) ambazo pia hazina camera.