kaka kuna setting za internet, WAP, web, nk kwenye mitandao yetu ya Tanzania. kama hauna setting za internet basi jua utapata matatizo mengi kama playstore kutofunguka, picha na video za Whatsapp hazidownload wakati msg zinakuja, opera inafunguka inabrowse ila app nyengine hazina internet etc
solution nenda setting halafu kwenye network click more network halafu mobile network halafu access point, angalia setting zako sio WAP? sio web? kwa uhakiki zaidi click add utengeneze setting mpya
connection name andika Tozy
APN andika internet
halafu click save
mbele ya setting mpya ya tozy utaona kiduara kiguse ili uiactivate hio setting.
hapo umemaliza angalia app zako kama zinafanya kazi