Wakuu bila shaka huu siyo msamiati mpya ila kama mjuavyo inawezekana jambo unalisikia miaka mingi tu na kulielewa juujuu tu ila ukitakiwa kulieleza kitaalamu ukakwama.
Nimepita ukurasa fulani mtandaoni jamaa anasema wanauza iPhone 15 Pro Max 512Gb ila copy (sh laki 4) ndo nkapaata mshawasha wa kutaka kujua wanaposema simu copy wanamaanisha nini hasa kitaalam?
Natanguliza shukrani.
Hizi huwa ni simu feki za android zinatumia mt6580. Mwambie adonwload CPU X ataona baadhi ya specs ambazo haziendeni na iPhone. Hata hiyo memori na Ram ni ya uongo pia