Simiyu Usione vyaelea ujue vimeundwa

Uchambuzi wenye hoja, Mhe. Mtaka anastahili kupongezwa sana. Ana kipawa cha uongozi.
 
Yaani nikiona watu wanatumia muda na nguvu nyingi kueleza walichokifanya,huwa napata shida kama wamefanya kitu kweli,kwanini mliyoyafanya yasijieleze yenyewe kwa watu,
Hapana hakuna aliyetumia nguvu nyingi, jambo kubwa ni kujifunza kutoka wa kiongozi huyu na
 
Hapana, Mtaka yupo vizuri. Hii taarifa sio sahihi. Tunamjua vizuri Mhe. Mtaka.
 
Unaweza kua sahihi au si sahihi kwenye baadhi ya sehemu. Ni wapi kwenye ilani ya ccm imeandikwa utekelezaji wa ujenzi wa nyumba za RAS na RC?

Kitu kibaya zaidi ni kusema uongo kua mwaka 2016 mtaka alikua na miaka 33; namfahamu sana Mtaka ni famili friend sana tokea utotoni na hapo Nyaumata kwake hua tunapiganae story sana..usisema uongo kwenye suala la umri kwa kiongozi wako.

Kitu kizuri kwa Mh Mtaka ni kutowaingilia ki majukumu wale wadau wa maendeleo katika mkoa wake kama Wakandarasi bali anawapa sana support na alipewa RAS Jumanne Sagini aliyegombea Ubunge Butiama.

Amna viwanda ulivyosema hapa Simiyu wenda kama unamaanisha Simiyu ya Japan.
 
Kabisa mtaka hakosi 40 to 50
 
Jambo jema, muda ni rafiki mzuri. Sote tusubiri naamini tutakuwa na furaha.
Baraza la Mawaziri lijalo litakuwa supa, na kuna uwezekano likaanza na watu wale wale na kumaliza na watu hao hao. Ni kwa sababu Mkuu sasa hivi ana orodha ya watu wengi sana ambao kwa sasa anawajua kikamilifu utendaji wao wa kazi. Kipindi anaingia mwaka 2015, yeye naye alikuwa Waziri kama wengine, na hakuwa na makundi kwa hiyo watu wote aliokuwa akiwachagua, alikuwa anachaguliwa na watu kwa kushauriwa. Safari ijayo atakuwa anachaguliwa, huku na yeye akiwa anashiriki katika kuamua chaguzi za watu hao. Naomba nibashiri kwa asilimia za juu kabisa kuwa Mh. Mataka atakuwa mmoja wao, assuming atapita ubunge
 
Hapana, pitia taarifa zote. Makala hii imeandikwa kwa kuzingatia mambo yote ya uandishi na taarifa zimetolewa katika vyanzo rasmi. Usitake kupotosha watu.
 
Inaweza kutokea, Mhe. Mtaka ni mfano wa kuigwa. Viongozi wengi hususani vijana wanaokua katika uongozi wanatakiwa kujifunza kutoka kwake. Ni kiongozi ambaye hufanya maamuzi kwa ajili ya maendeleo jumuishi, hafanyi kwa ajili ya kuwafurahisha watu wachache. Anazingatia weledi, nidhamu, uadilifu, bidii na maarifa katika kazi na utumishi wake wa umma. Mwenyezi Mungu amuongoze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…