Mkuu mambo mengi uliyoyazungumza ni ya kujenga ufahamu wa walio na nafasi ya kuleta mabadiliko katika timu. Tatizo la kushabikia mambo lipo kila mahali hata katika mambo ambayo hayahitaji ushabiki. Matawi nayo yanatumika na wahusika kutimiza malengo yao.wakati rage akiwaita wanachama wa simba mbumbumbu wengi tuliona kawatukana ila ukweli aliwaambia ingawa hayupo.Wanachama walipaswa kuwaoji wakina Aveva kwanini wananshindwa kuipa timu mafanikio, kama tatizo ni pesa waelez vitega uchumi likiwemo jengo la msimbazi na mauzo ya jezi yanaenda wapi.Wanachama wengi wanamshabikia dewji kununua simba hisa 51% kwa bilioni 20 wakati hakuna chombo chochote kilichokaa na kuthibitisha thamani halisi ya simba ikiwa pamoja na fanbase yake.Wameshindwa kumuuliza dewji nini kilimshindwa afrika lyon mpaka akaiuza na je simba ikimshinda hatachukua maamuzi hayohayo.Dewji anatumia umbumbu wa wananchama wa simba kutekeleza malengo yake kama ka kweli anaipenda simba na yeye ni mwanachama mbona kikao cha jana hakuhudhuria?wanachama wameshindwa hata kuhoji taarifa ya fedha ingawa ilikuwa na mapungufu mengi kisa kudai timu auziwe dewji.wanabaki kulaumu wazee wa simba wakati hawajui wao ndio walianzisha hiyo timu na mpaka leo bado ipo.
Mkuu rodrick alexander, hapo kwenye red umeandika maneno ya maana sana.wakati rage akiwaita wanachama wa simba mbumbumbu wengi tuliona kawatukana ila ukweli aliwaambia ingawa hayupo.Wanachama walipaswa kuwaoji wakina Aveva kwanini wananshindwa kuipa timu mafanikio, kama tatizo ni pesa waelez vitega uchumi likiwemo jengo la msimbazi na mauzo ya jezi yanaenda wapi.Wanachama wengi wanamshabikia dewji kununua simba hisa 51% kwa bilioni 20 wakati hakuna chombo chochote kilichokaa na kuthibitisha thamani halisi ya simba ikiwa pamoja na fanbase yake.Wameshindwa kumuuliza dewji nini kilimshindwa afrika lyon mpaka akaiuza na je simba ikimshinda hatachukua maamuzi hayohayo.Dewji anatumia umbumbu wa wananchama wa simba kutekeleza malengo yake kama kweli anaipenda simba na yeye ni mwanachama mbona kikao cha jana hakuhudhuria?wanachama wameshindwa hata kuhoji taarifa ya fedha ingawa ilikuwa na mapungufu mengi kisa kudai timu auziwe dewji.wanabaki kulaumu wazee wa simba wakati hawajui wao ndio walianzisha hiyo timu na mpaka leo bado ipo.
Hio bil 20 hata GOODWILL ya simba pekee haitoshi, sembuse total market value ya Simba, huo ni mzaha mtupu
Kuna kitu hujakielewa vizuri. Tatizo la Simba liko kwenye suala la timu iendeshweje, kampuni au hivi hivi na wanachama?
Watu wengi wanataka timu ijiendeshe kwa mfumo wa kampuni ambapo hisa zitanunuliwa na yeyote mwenye kutimiza masharti na kisha mwenye nyingi ndie atakayekuwa na sauti ya mwisho. Hapa anaweza akawa ni Dewji au mtu yeyote mwenye mpunga.
Pili umetolea mfumo wa Yanga, huko umepotea kabisa kwa sababu Yanga haina mfumo kama huu wanaotaka kuanzisha Simba. Yanga wana kiongozi mwenye fedha nyingi ambae hana hisa wala si mmiliki ila anatoa fedha yake mfukoni kusaidia mambo yaende. Ni hisani tu anafanya, akiondoka au siku akishindwa uongozi ndio itakuwa mwisho wa kula fedha zake.
Mfumo wa Simba kama watafanikiwa ndio mfumo wa kisasa na timu nyingi duniani zinautumia, na ikitokea mtu amebadili mawazo anauza hisa kwa mtu mwingine
Nenda mahakamani...sio unabaki kuongea humu kwa kiburi...mabadiliko ni lazimaHuyu Dewji dawa yake ni mahakamani tu...
manake anatumia njaa za watu wachache kuleta usanii
Kuna MTU yeyote aliyeonesha nia ya kutaka timu za ya Mo...au mnaongea tu thamani ya simba ni zaidi ya bil 20 wakati rais wa Simba amesema thamani ya Mali za simba hazifki hata bil 5Mbadiliko kwa utaratibu sio kwa usanii..
Sioni kama kuna shida yoyote kwani hakuna chochote anachokabidhiwa mtu bila kuwepo terms and condition za kisheria.Hivi vitu vitaenda kisheria na makubaliano ya kisheria lazima yawepo.Mbadiliko kwa utaratibu sio kwa usanii..