Tatizo ni kocha na Mugalu wake, utadhani kamroga. Hafanyi lolote ndani na hamfanyii sub.
Wakati tunawa-miss Chama na Konde Boy, pengo lingine ni la Sven ambalo haliongelewi sana. Tangu Sven aondoke kiwango cha uchezaji kimeshuka sana na kutegemea sana kujaza ma-striker mfumo ambao tija yake ndogo kwani hawako clinical na hupoteza nafasi nyingi za magoli.
Bila kupepesa macho, Gomes hatufai Simba na mwaka huu hatuvuki makundi. Wanasema mpira ni biashara matokeo yake ndio haya. Kwa mimi nasema mpira ni wachezaji. Biashara haichezi mpira. Leo hii timu aliyokwenda Chama wakisema turudishieni pesa yetu na mumchukue Chama wenu, wana Simba wengi kama sio wote watasema tupeni Chama wetu. Biashara tulifanya lakini timu tuliiharibu. Afadhali tungekomaa na Chama, Miqueson aende. Pengo la Chama litatukaa vichwani kwa muda mrefu sana na hasa ukizingatia kiuwezo Bwalya ni kama nusu ya Chama.
Mwaka huu Simba itabidi ijihadhari sana kwani kila timu itakuja imepania kwa kudhani kuwa Simba sasa ni rahisi kufungika kutokana na kutokuwepo kwa wachazaji hao wawili.
Kwa mtazamo wangu mimi, ubingwa mwaka huu ni 40% Simba, 30% Yanga na 30% Azam. Na point za ubingwa mwaka huu hazitovuka hamsini kwa timu yoyote ile na kutakuwa na funga nikufunge nyingi tu msimu huu na ubingwa utapatikana katika mechi mbili za mwisho na sio kama tulivyozoea mechi tano au sita kabla. Nauona ushinfani wa nguvu msimu huu.