Simba bado ni timu bora kuliko zote tz. Kelele zote hz ni kutokana na ubora wa timu ya simba. Ni wazi hata yanga mlishangilia droo na simba iweje mbao wasishangilie.
Bado naamini simba ndiyo bingwa.
Endelea kuamini hivyo maana ni haki yako ya kikatiba.
Nikukumbushe tu: siyo lazima kila kitu unachoamini ndivyo kilivyo! Hata Wapagani wanaamini miungu yao ya mawe, miti, wanyama n.k wakati Mungu ni mmoja tu aliyeumba mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo (Kutoka 20:11).
Toka ninywe chai na ule mgoli wa mbao mpaka sasa sijala kitu na wala sihisi njaa kuna jamaa kaniambia naweza kaa siku 3 bila kula kitu,asanteni sana mbao
Leo sijalipa nauli kwenye vyombo vyote vya usafiri nilivyopanda,kuanzia Mwendokasi mpaka Bajaji. Nikiombwa nauli nilikuwa natoa simu yangu na kuonyesha lile goli la Maganga kisha wananiambia usitoe nauli hiyo ndio nauli yako.