Simba na jezi za Adidas

Nakapanya

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Posts
2,096
Reaction score
709
Kuna wwakati jezi za simba zilikuwa na logo ya adidas,swali ninalojiuliza mi kuwa je simba walidhaminiwa na adidasi ama ilikuwaje?
 
Mkuu Nakapanya,

Simba haijawahi kuwa na mkataba hai wowote wa udhamini wa vifaa vya michezo. Mwaka 2007 waliwahi huingia mkataba na Adidas kupitia wakala wao aliyepo nchini Malawi, kwa sababu zisizofahamika mkataba ule haukuwahi kutekelezwa. Jezi wanazofaa sasa hivi ni ambazo wanapewa na wadhamini wa Ligi Kuu, Vodacom na zingine ambazo huwa wanapewa na wadhamini wao magumashi, Kampuni ya Bia (TBL).
 
Last edited by a moderator:
Kuna wwakati jezi za simba zilikuwa na logo ya adidas,swali ninalojiuliza mi kuwa je simba walidhaminiwa na adidasi ama ilikuwaje?

Adidas hawajui kama kuna soka inachezwa Tanzania, wanachojua wao pande za bongo watu bado wanapiga ndege kwa manati tu.
 
je hii jezi ya Taifa Stars yenye nembo ya adidas kifuani pia ni magumashi?
 
Iko siku kila mtu ataishangilia Simba.
Nalog off
 
kwahiyo simba wanaitangaza adidas bure?
 
je hii jezi ya Taifa Stars yenye nembo ya adidas kifuani pia ni magumashi?

Ndio, tena magumashi makubwa tu, Starz walikuwa na mkataba wa mavazi na kampuni moja ya MArekani, ilikuwa inaitwa +One na mkataba huo ulikuwa wa miaka minane. Haijulikani mkataba ule uliishia wapi ghafla tukaona wanavaa jezi za UhlSports kwa hisani ya Kassim Dewji ambae nasikia ndio anawadhulumu vilabu vikubwa vya KAriakoo kwa kuuza jezi za magumashi kwao.

Hizi wanazovaa sasa hivi zilitolewa kwa msaada na CAF, nilimuuliza muheshimiwa Rais akajibu eti huo mkataba waliukuta umeshasainiwa kwa hiyo hawana budi kuuheshimu.

Ni kaupuuzi fulani kanafanywa kwa makusudi huku watu wakiwa wanafahamu.
 
je hii jezi ya Taifa Stars yenye nembo ya adidas kifuani pia ni magumashi?

Viol na Mphamvu jezi zinazovaliwa na Taifa Stars zimebandikwa nembo halali ya Adidas kwa mujibu wa mkataba kati ya TFF, Adidas na CAF. Anayebishia au kubeza ukweli huu bila shaka ana lake jambo!

By the way Mphamvu kwa nini unabeza mkataba wa Simba SC na TBL mkataba wenye thamani ya nusu bilioni kwa mwaka? Inasaidia nini kuwabeza wafadhili ambao wana support mpira nchini mwetu?

TFF tunalilia waongezeke ninyi mnawabeza, that is a disfavour and a disservice to Tanzanian football.
 
Mkuu Jamal Malinzi,hapo juu Mphamvu ameeleza ''Starz walikuwa na mkataba wa mavazi na kampuni moja ya MArekani, ilikuwa inaitwa +One na mkataba huo ulikuwa wa miaka minane. Haijulikani mkataba ule uliishia wapi ghafla tukaona wanavaa jezi za UhlSports kwa hisani ya Kassim Dewji ambae nasikia ndio anawadhulumu vilabu vikubwa vya KAriakoo kwa kuuza jezi za magumashi kwao.
Je huo mkataba na kampuni ya +one ya marekani ni kweli,na huo mkataba ulishaisha?
 
Last edited by a moderator:

Ndugu Rais, ninazo taarifa kuntu kabisa kuwa jezi zinazovaliwa na Starz ni zina nembo halali ya Adidas na zimetolewa 'MSAADA' kupitia programu maalumu ya CAF na Adidas kusaidia vifaa kwa timu ambazo hazina udhamini kwa sasa, hivyo hisia zako kuwa ninabisha si KWELI.

Ukakasi ninaoupata ni timu ya Taifa ambayo ina uwezo wa kuuza jezi za 'replica' hata milioni moja (kigezo kikubwa cha kupata udhamini kutoka kwa makampuni ya vifaa vya michezo) kwa mwaka kuingizwa katika kundi hili la wanaosaidiwa.

Nilikuuliza kitambo kidogo kuhusu hili ukanijibu kuwa uongozi wako ulikuta mkataba huu umeshasainiwa na uongozi uliopita, jukumu leu ni kuuheshimu. Ajabu ni kuwa kiwango cha jezi mnachopewa kwa mwaka kikiisha mnalazimika KUNUNUA, kwa hao hao ambao wanawasaidia, sijui kwa bei gani (nisahihishe kama nimekosea). Kama suala lina maslahi kwa TFF na nchi, kwanini msivunje huo mkataba wa kihuni (kama mlivyovunja wa mwalimu Kim Poulsen) ambapo Adidas wanawafanyia biashara ya lazima kwa jina la misaada, tena msaada ambao upo ndani ya uwezo wenu?

Hakuna mahali ambako nimebeza udhamini wa TBL katika uzi huu, ninayo madai mengine juu ya udhamini wa TBL kwa Simba na Yanga lakini si haya ya leo. Nilichofanya ni kumweleza mtoa mada 'sera' ya mavazi ya Simba ikoje na ni wapi wanakopata viwalo vyao kwa sasa.

Kwenye mada yangu nimemtaja Kassim Dewji ambaye ni mfanyabiashara wa jumla wa vifaa vya michezo, kama liko ndani ya uwezo wako unaweza kutoa maoni yako kumhusu.

Natanguliza shukrani.
 
TFF yapata mkataba mnono wa Sh5.85bilioni toka Marekani - Tanzania Sports
 
Last edited by a moderator:
Hii ndio jezi iliyokuwa ikivaliwa wakati wa mkataba husika...
 
Last edited by a moderator:
it seems mphamvu unajua vizuri hizi ishu,endelea kutujuza mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…