Namshakende
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 844
- 2,184
Hapa ni unamsema Ateba, Kibu, Mukwala na yule Mwanariadha wa DRC (Mpanzu).Ni dhahiri Sisi mashabiki wa Simba tuna mapenzi makubwa na timu yetu na tunatamani kuona mafanikio endelevu. Katika kutafakari mwenendo wa timu, ni muhimu kuangalia kwa jicho la tatu aina ya wachezaji ambao watatufikisha kwenye malengo yetu.
Wakati tunawashuhudia wachezaji wengi wa Simba wakitumia nguvu, kasi, na kujituma uwanjani, kuna wasiwasi kuhusu uwezo wao wa kufanya maamuzi sahihi na kuwa na ubunifu katika eneo la mwisho. Mara nyingi, tunaona juhudi kubwa zinazokosa umakini na maarifa yanayohitajika ili kuleta madhara kwa timu pinzani.
Tunahitaji kukiri kuna pengo katika akili ya soka kwa baadhi ya wachezaji wetu. Tunashuhudia wachezaji ambao wanategemea zaidi nguvu na mikimbio kuliko uwezo wa kufikiri na kupanga mashambulizi kwa ufanisi. Matokeo yake, tunajikuta tukipoteza nafasi nyingi na kushindwa kuvunja ulinzi wa wapinzani kwa urahisi.
Ni wakati sahihi kwa uongozi wa Simba kuweka mkazo katika kusajili wachezaji wenye akili kubwa ya soka, kama tunavyoona kwa Clatous Chama, Pacome, Maxi, Fabrice , e.tc . Wachezaji wenye uwezo wa kuona nafasi, kupiga pasi zenye uhakika, na kufanya maamuzi sahihi chini ya presha ndio watakaotupeleka kwenye mafanikio makubwa.
Tusipuuze umuhimu wa kuwa na wachezaji wenye uwezo wa kufikiri na kutumia akili zao uwanjani. Ni muhimu kuwekeza katika wachezaji ambao wanaweza kuleta ubunifu na mbinu mpya katika safu yetu ya ushambuliaji.
Tunahitaji timu ambayo ina mchanganyiko wa nguvu na akili. Kuwa na wachezaji wenye uwezo wa kufikiri na kutenda kwa usahihi ndio tutaweza kushinda mechi na kufikia malengo yetu.
Simba inahitaji mageuzi katika aina ya wachezaji ili kuhakikisha tunakuwa na timu imara na yenye uwezo wa kushindana katika ngazi zote(Yanga) . Ni wakati wa kuwekeza kwenye akili ya soka kwa manufaa ya timu yetu.
Wanatumia Nguvu kubwa , matumizi ya akili ni sifuri kabisa.Hapa ni unamsema Ateba, Kibu, Mukwala na yule Mwanariadha wa DRC (Mpanzu).
Kama vipi tubadilishane wachezaji. Wa simba waende Yanga, na wa Yanga waende simba.
Sijui nikujibu wewe mwendawazimu unayefahamika na kila mtu humu jukwaani! Sijui ni kupotezee tu!Unashinda JF kuandika utumbo tu.
UNASIKITISHA SANA.
Dogo una msongo wa mawazo uliopitiliza! Na haihitaji mtu awe na elimu kubwa kukutambua kama dishi lako kichwani limeyumba kutokana tu na msongo mkubwa wa mawazo ulio nao.kutwa Kushinda jf kuandika pumba tu.
Inaonekana Maisha yangu unayajua kuliko hata mimi mwenyewe ???
Sipendi kuandika matusi na Upumbavu kama wewe usiye na Akili wala Elimu.
Idiot.
Sijui nikujibu wewe mwendawazimu unayefahamika na kila mtu humu jukwaani! Sijui ni kupotezee tu!
Ila kwa taarifa yako mimi nipo humu jukwaani kwa ajili ya ku refresh tu akili yangu! Na siyo kupunguza msongo wa mawazo unaotokana na maisha magumu kama ilivyo kwako wewe. Sawa. So relax, ok?
Kiukweli hata Mimi naumia kuona tumepata bahati ya kukutana na timu Ile harafu tukakosa ushindi, mocha Hana mipango anaishi kwa kubahatishaSimba sio mbovu ila inakutana na timu imara zaidi yake hapo ndio mafuta na maji vinajitenga
Kabisa ujue sisi Simba ni Mbumbumbu na tunawahi kusahau sana ukiangalia Yanga Ina wachezaji waliojichokea kama Pacome , mzize na Dube hata kupiga shuti hawawezi lakini bado wanashinda kwa kuhonga marefa..Ndugu zangu wa simba, shida siyo wachezaji! Shida ni GSM anatuharibia ligi yetu. Hata kule kufungwa na Al Masry, chanzo ni GSM! Hili jambo hatutakiwi kulisahau hata sekunde moja. GSM anadhamini timu 7 kwenye ligi yetu.