Sijajua ni kwanini Marais wanapata shida kupata Mawaziri miongoni mwa wabunge wa kuchaguliwa wa CCM

La maana raisi acheze na zile nafasi zake za kuteuwa wabunge. Ateuwe watu vichwa na awape wizara nyeti. Aangalie kwa makini wale waliochaguliwa na wananchi kama wapo vichwa, wapewe uwaziri.
 
Sio rahisi kupata Watu wa maana miongoni mwa Wabunge wa majimbo kwa kuwa Mchakato wa kuwapata ni wa kihuni sana

Imagine Mtu kama Prof Assad anaweza kweli kwenda kutenegeneza Majungu na makundi ya Mitandao majimboni sijui kukesha kwa Wajumbe wa Serikali za mitaa, sijui kuhonga honga wapiga kura, kujipendekeza kwa Wajumbe, Wajumbe wa NEC na Kamati kuu

Ukishapitishwa na chama uanze sasa heka heka na mikakati ya kupanga Mawakala wako, kununua wa wapinzani wako,

Siku ya kupiga kura ununue zile hot pot kubwa sana za chakula, wakati wa Lunch sehemu kubwa ya hot pot inajazwa kura feki na kiugali kama ngumi tu…Wakala anakula Ugali wake huku akikamilisha Mikakati ya kuchomeka zile kura za kwny hot pot kwenye sanduku akishashiba ugali

Tusahau Watu smart Bungeni hasa kwa Wabunge wa majimbo wa kutoka pande zote za vyama…usipokuwa Muhuni huwezi kuwa Mbunge wa jimbo zama hizi
😁
 
Hivi inakuwaje bungeni una wabunge tena wa chama chako zaid ya 300 halaf unateua mtu kutoka nje ya bunge unampa uwaziri direct?

Ina maana wote wale walioko kule ndani hawafai? Hakuna mwenye vigezo unavyotaka?

Huu utaratibu siuelewagi naonaga kama dharau
 
Kwenye somo la statistics ukiwa na idadi ya machungwa elfu moja na ukataka kujiridhisha kwamba ni matamu na yana maji mengi ili uyanunue na kwenda kutengeneza juice itakulazimu uchukue sample ya machungwa 50 (ambayo ni 5% ya machungwa yote) ikitokea hayo machungwa 50, ambayo umeyachagua randomly, ni makali na hayana maji maana yake ni kwamba tatizo kuu liko kwenye huo mzigo wa machungwa elfu moja...
Hayo machungwa 50, unayala yote!! Kazi
 
Hayati Magufuli alipata hii shida ikabidi akope wabunge wa Chadema akina Mwita Waitara na Dr Mollel na kuwapa uwaziri.

Na sasa ni kama tatizo bado lipo Waziri wa ulinzi bado hajateuliwa labda mama Tax ataokoa jahazi kwa kwenda wizara ya tax na yule mwanayanga kwenda ulinzi.

CCM tujitahidi kuchagua wabunge wenye sifa siyo hawa akina Kibajaji, Babu Tale Kinanasi, Tabasamu, Musukuma Jah people nk..nk

Nawatakia Sabato yenye baraka!
Katika hii list Msukuma mtoe hapa,ana akili kuwazidi asilimia 75 ya Wabunge wote.
 
Mfumo wetu wa kupata wabunge ni mbovu mtu anayejua kupiga domo na mwenye fedha anahonga wajumbe wa CCM halafu wanampitisha wakienda kwenye uchaguzi mkuu TISS na Polisi wanawapitisha kuwa wabunge sasa hapo unategemea kupata mtu wa maana kwenye nafasi hiyo? Walihangaika kupitisha watu wenye uwezo mdogo kuwa wabunge hatimaye wamekosa watu wa kuwateua kuwa mawaziri.

Watu kama Babu Tale,Msukuma,Kibajaji,Kigwangala,Zungu,Gwajima na wengineo hawakustahili hata kuwa Wenyeviti wa vijiji.Uwezo wao wa kupiga porojo na kuhonga vijisenti ndiyo umesababisha kufika hapo walipo.
Gwajima na Msukuma wana akili nyingi zaidi ya mawaziri.
 
Hayati Magufuli alipata hii shida ikabidi akope wabunge wa Chadema akina Mwita Waitara na Dr Mollel na kuwapa uwaziri.

Na sasa ni kama tatizo bado lipo Waziri wa ulinzi bado hajateuliwa labda mama Tax ataokoa jahazi kwa kwenda wizara ya tax na yule mwanayanga kwenda ulinzi.

CCM tujitahidi kuchagua wabunge wenye sifa siyo hawa akina Kibajaji, Babu Tale Kinanasi, Tabasamu, Musukuma Jah people nk..nk

Nawatakia Sabato yenye baraka!
Wenye sifa za kuwa ubunge wanaachwa wanapewa wenye kujua kupiga pambio mradi kama anajua kusoma na kuandika tu. Kwa nini watunga sheria wanakuwa darasa la saba wakati huo anayetekeleza lazima awe na degree.
 
They choose people of their own interest and not material ones. It is a personal interest full stop
 
Hayati Magufuli alipata hii shida ikabidi akope wabunge wa Chadema akina Mwita Waitara na Dr Mollel na kuwapa uwaziri.

Na sasa ni kama tatizo bado lipo Waziri wa ulinzi bado hajateuliwa labda mama Tax ataokoa jahazi kwa kwenda wizara ya tax na yule mwanayanga kwenda ulinzi.

CCM tujitahidi kuchagua wabunge wenye sifa siyo hawa akina Kibajaji, Babu Tale Kinanasi, Tabasamu, Musukuma Jah people nk..nk

Nawatakia Sabato yenye baraka!
Wabunge wenu walioingizwa kijambazi mjengoni kwa kura za kwenye mabegi ni vilaza wa kutupwa, imagine babu Tale naye ni Mbunge upuuzi mtupu
 
Mmeacha watu wanaofit wapo wengi Sana mmechagua viazi
Wametujazia hivi mjengoni
20210911_094721.jpg
 
Hayati Magufuli alipata hii shida ikabidi akope wabunge wa Chadema akina Mwita Waitara na Dr Mollel na kuwapa uwaziri.

Na sasa ni kama tatizo bado lipo Waziri wa ulinzi bado hajateuliwa labda mama Tax ataokoa jahazi kwa kwenda wizara ya tax na yule mwanayanga kwenda ulinzi.

CCM tujitahidi kuchagua wabunge wenye sifa siyo hawa akina Kibajaji, Babu Tale Kinanasi, Tabasamu, Musukuma Jah people nk..nk

Nawatakia Sabato yenye baraka!
Wengi huangushwa na "Upekuzi" aka vetting!
 
Back
Top Bottom