Hivi sensa ya mwaka huu ina tofauti gani na zilizopita? Toka tupate uhuru hii itakuwa sensa ya nne au ya tano na huko nyuma watu walihesabiwa bila matatizo. Tena makarani walikuwa ni wanafunzi wa shule za sekondari. Mwaka huu sensa imefanywa kama vile ni kitu kipya. Naweza kutowashangaa vijana ambao hii ndiyo sensa yao ya kwanza lakini kwa watu wazima kuhojihoji na madai yasiyo na msingi ni ujinga.